Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Senegal: Wanasiasa wachukuwa msimamo katika hali ya kutokuwa na uhakika

Vuguvugu la kiraia nchini Senegal la Aar Sunu linashikilia kuwa uchaguzi wa urais lazima ufanyike kabla ya Aprili 2, na kukataa muda usiokuwa na uhakika ulioongezwa na mkuu wa nchi licha ya mzozo uliosababishwa na kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais, vmaafisa wamesema.

Rais Sall wakati wa hotuba yake kwenye televisheni.
Rais Sall wakati wa hotuba yake kwenye televisheni. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Rais Macky Sall kuzungumza Alhamisi jioni, sasa kazi kubwa iko mikononi mwa wadau wa siasa na kijamii, ikiwa ni pamoja na wagombea na mashirika ya kiraia. Ni juu yao kusema iwapo watakubali kusitisha tarehe ya mazungumzo ambayo Bw. Sall alisema anataka kutekeleza siku ya Jumatatu na Jumanne, kwa matumaini ya kufikia makubaliano siku ya Jumanne jioni.

Tulikuwa tunamngoja (rais)" kwa tarehe hii, "mengine yanayosalia, maneneo tupu yasiyo kuwa na maana yoyote",  Aar Sunu Election ("Tuhifadhi uchaguzi wetu"), vuguvugu la kiraia limeliambia shirika la habari la AFP. Mazungumzo yaliyopangwa na Rais Sall "hayana maana," limeongeza.

Wengi wa wadau hawa wa siasa walichukua muda kutafakari maneno ya Mkuu wa Nchi, kwa shinikizo nyingi za kitaifa na kimataifa kuandaa uchaguzi huu haraka iwezekanavyo, na kuahirishwa kwake Februari 3, kwa gharama ya moja ya migogoro mikubwa zaidi ambayo nchi yake imepitia kwa miongo kadhaa. Wasenegal walitakiwa kupiga kura siku ya Jumapili wikendi hii.

Uahirishaji huo, uliolaaniwa kama "mapinduzi ya kikatiba" na upinzani, ulisababisha ghasia katika maoni ya umma na maandamano ambayo yalisababisha vifo vya watu wanne. Baraza la Katiba hatimaye lilitoa uamuzi dhidi ya Bw. Sall na Bunge la Kitaifa.

Baada ya kura hii ya turufu ya kikatiba, na licha ya matarajio ya pamoja ya ufafanuzi katika wapiga kura ambao kwa kiasi kikubwa unahusishwa na zoezi la kidemokrasia na heshima kwa kalenda, Rais Sall hakuacha tu tarehe hiyo ikisubiri, lakini aliona kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba Wasenegal hawatapiga kura hadi muhula wake utakapomalizika rasmi tarehe 2 Aprili.

Bw. Sall, aliye madarakani tangu mwaka wa 2012, alijibu wasiwasi ulioenea na kuondoa shaka kwamba kweli ataacha wadhifa wake Aprili 2, tarehe ambayo muhula wake wa pili utamalizika rasmi.

Macky Sall ambaye alihalalisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais kwa kuhofia maandamano na ghasia za kabla na baada ya uchaguzi kama vile matukio mabaya ambayo nchi hiyo iliyoshuhudiwa mnamo mwezi Machi 2021 na Juni 2023, alisisitiza nia yake ya kutunza amani na kuboresha maridhiano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.