Pata taarifa kuu

ECOWAS: Rais wa Tume atangaza kuondolewa kwa vikwazo vingi dhidi ya Niger

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wameamua kuondoa sehemu ya vikwazo dhidi ya Niger "mara moja", ametangaza rais wa Kamisheni ya kanda yajumuiya hiyo Jumamosi hii huko Abuja. Vikwazo viliwekwa kwa Niamey baada ya utawala wa kijeshi kuchukua mamlaka na kumpindua Rais aliyechaguliwa Mohamed Bazoum mwezi Julai. Mipaka na anga zitafunguliwa tena, imeamuliwa mwishoni mwa mkutano huu usio wa kawaida.

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, na Omar Touray, Rais wa Tume ya ECOWAS, katika kikao kisicho kuwa cha kawaida cha wakuu wa nchi na serikali wa sjumuiya hiyo, mjini Abuja Jumamosi hii, Februari 24, 2024.
Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, na Omar Touray, Rais wa Tume ya ECOWAS, katika kikao kisicho kuwa cha kawaida cha wakuu wa nchi na serikali wa sjumuiya hiyo, mjini Abuja Jumamosi hii, Februari 24, 2024. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Abuja, Moïse Gomis

Kuondolewa kwa vikwazo vya shughuli za kifedha na benki, mwisho wa vizizi vya nishati, kurejeshwa kwa safari za ndege za kibiashara kuondoka na kutua nchini Niger, mwaliko rasmi uliozinduliwa kwa viongozi wa tawala za kijeshi wa nchi hizo nne ambao hadi sasa wamesimamishwa kwa vikao hivi vya mkutano wa wakuu wa nchi na serikali...

Kwa hivyo ECOWAS inaondoa takriban vikwazo vyake vyote dhidi ya Niger, na inaomba kuachiliwa mara moja kwa Mohammed Bazoum. Taarifa ya mwisho kwa vyombo vya habari kutoka kwa ECOWAS haielezi wazi iwapo kuondolewa kwa vikwazo kunatokana na ombi la kuachiliwa kwa Bw. Bazoum.

Majadiliano kati ya wakuu wa nchi wa Muungano wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU) hayajaisha. Wakuu wa nchi za Togo, Benin, Senegal, Côte d'Ivoire na Guinea-Bissau wanakamilisha rasimu ambayo itaunda pendekezo la majibu kamili na majibu ya sasa ya mzozo wa wazi kati ya ECOWAS kwa upande mmoja na kwa upande mwingine Burkina Faso, Mali na Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.