Pata taarifa kuu

Mamia ya Wasenegali waandamana kwa ajili ya uchaguzi wa urais bila kuchelewa

Mamia kadhaa ya raia wa Senegal waliandamana siku ya Jumamosi mjini Dakar kumtaka mkuu wa nchi kuandaa uchaguzi wa rais kabla ya mwisho wa mamlaka yake Aprili 2, baada ya kuahirisha hadi tarehe ambayo bado haijajulikana.

Waandamanaji wa Senegal kutoka jukwaa la mashirik ya kiraia la AAR SUNU waandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari 25 huko Dakar, Senegal Februari 17, 2024.
Waandamanaji wa Senegal kutoka jukwaa la mashirik ya kiraia la AAR SUNU waandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari 25 huko Dakar, Senegal Februari 17, 2024. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Wasenegal walipaswa kumchagua rais wao wa tano siku ya Jumapili Februari 25. Rais Macky Sall alianzisha sintofahamu na mvutano mnamo Februari 3 kwa kuagiza kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais kwa dakika ya mwisho.

Baraza la Katiba labatilisha uamuzi wa rais

Lakini Wasenegal hawajui ni lini watapiga kura na ikiwa itakuwa kabla au baada ya Aprili 2, tarehe rasmi ya kumalizika kwa muhula wa Bw. Sall, ambayo itakuwa hali isiyokuwa ya kawaida. Kutokuwa na uhakika kumeendeleza mvutano. Vuguvugu kubwa la kisiasa na kiraia linataka kura ifanyike bila kuchelewa.

Mamia ya watu wamekusanyika kwa mwito wa muungano wa upinzani F24 kwenye eneo kubwa la mchanga katika eneo lenye watu wengiw katia mji wa Dakar. Katika kelele za filimbi na pembe, wakionyesha bendera za kijani, dhahabu na nyekundu za Senegal, walitaka kura ifanyike. Vuguvugu la kiraia la Aar Sunu ("Hebu tuhifadhi uchaguzi wetu") ulitoa wito kwa watu kujiunga na maandamano, huku wakitaka kudumisha uhuru wao wa kisiasa.

Ombi hilo lilienea hadi kuachiliwa kwa wapinzani Ousmane Sonko na Bassirou Diomaye Faye, ambao wafuasi wao ndio walioonekana zaidi na wenye kelele miongoni mwa umati. Iligeuka kuwa maandamano dhidi ya utawala.

"Tunataka uchaguzi, Macky Sall dikteta, Diomaye mooy Sonko" (Diomaye, Sonko, vita sawa kwa kiouolof), waandamanaji waliimba.

"Ninaandamana kwa jambo moja tu: Sonko aachiliwe. Macky Sall aache kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji," Ibrahima Niang, mkusanya takataka mwenye umri wa miaka 34, ameliambia shirika la habari la AFP, akiwa amebeba moja ya mabango mengi ya Bw. Sonko yaliyoonyeshwa siku ya Jumamosi.

Manispaa ya mji iliidhinisha maandamano hayo huku mamlaka ikipiga marufuku mikutano mingi ya upinzani katika mazingira ya mvutano katika miaka ya hivi karibuni. Hivi karibuni serikali ilihibitisha nia yake ya kutuliza mvutano. 

Manispaa ya mji pia meidhinisha maandamano yaliyopangwa alasiri na kambi ya "Macky" kumuunga mkono Mkuu wa Nchi. Wakati huohuo, vuguvugu la Aar Sunu linawaalika wakazi wa Dakar kukusanyika na chakula au vinywaji kwa kile kinachokusudiwa kuwa "sherehe ya kuondoka" ya Rais Macky Sall.

Senegal, ambayo inasifiwa kwa uthabiti na mazoea yake ya kidemokrasia licha ya kukumbwa na machafuko makubwa ya kisiasa siku za nyuma, imeendelea kutumbukia katika moja ya migogoro mibaya zaidi tangu uhuru wake mwaka 1960.

Uamuzi wa Rais Sall wa kuahirisha uchaguzi huo, uliolaaniwa na upinzani kama "mapinduzi ya kikatiba", ulichochea maandamano ambayo yalisababisha vifo vya watu wanne na kusababisha watu kadhaa kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.