Pata taarifa kuu

Rais Sall afungua 'mazungumzo' kumaliza mgogoro nchini Senegal

Rais wa Senegal Macky Sall ameleta pamoja idadi kadhaa ya wadau wa kisiasa na kijamii siku ya Jumatatu kujaribu kupata makubaliano juu ya tarehe ya uchaguzi wa urais, lakini wahusika wakuu walitangaza kwamba watasusia mazungumzo hayo.

Rais Sall alihalalisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais kwa hofu yake kwamba uchaguzi unaoshindaniwa ungezusha ghasia mpya baada ya zile zilizoshuhudiwa 2021 na 2023.
Rais Sall alihalalisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais kwa hofu yake kwamba uchaguzi unaoshindaniwa ungezusha ghasia mpya baada ya zile zilizoshuhudiwa 2021 na 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Bwana Sall amejipa siku mbili, Jumatatu na Jumanne, kutafuta njia ya kutoka katika mzozo ambao nchi inapitia, moja ya shida kubwa zaidi katika miaka 64 ya uhuru, tangu alipoagiza mnamo Februari 3 kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais ambao ulikuwa ifanyike siku ya Jumapili. Amewaalika kwenye "mazungumzo" haya huko Diamniadio, mji mpya karibu kilomita thelathini kutoka mji mkuu wa Dakar, wagombea walioidhinishwa mwezii Januari na Baraza la Katiba, wale ambao hawakuidhinishwa, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, viongozi kidini na kimila, ofisi ya rais imebainisha.

Rais Sall, aliyechaguliwa mwaka wa 2012 na kuchaguliwa tena mwaka wa 2019, hatawania katika kinyang'anyrio cha urais. Lakini anasisitiza juu ya mgawanyiko ambao mchakato wa kabla ya uchaguzi umeongezeka kulingana na rais huyo na haja ya "maridhiano" kwa ajili ya utulivu ambao nchi yakeimekuwa ikishuhudia. Analenga "makubaliano" mwishoni mwa mazungumzo ambayo, alisema siku ya Alhamisi, yatajikita kweye tarehe mpya ya uchaguzi wa urais, lakini pia baada ya Aprili 2, tarehe rasmi ya mwisho wa muhula wake.

Aidha washiriki wakubaliane tarehe na "atachapisha" mara moja agizo ya kuwaita wapiga kura, au atalipeleka suala hilo kwa Baraza la Katiba, ili liamue, alisema siku ya Alhamisi.

Wagombea 16 tu kati ya 19 walioidhinishwa na Baraza la Katiba ndio ambao walisema hawatashiriki mazungumzo hayo. Vuguvugu la Aar Sunu ("Hebu tuhifadhi uchaguzi wetu"), linalodai kukusabya zaidi ya mashirika na watu mia moja kuungana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi, pamoja na majukwaa mengine ya raia, limsema halitashiriki mazungumzo hayo.

Wanaunda safu kubwa ambayo inadai kwamba uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo, na kabla ya Aprili 2. Baadhi yao wana wasiwasi kuhusu athari ya pengo kubwa kwenye nafasi ya rais baada ya muhula wake kumalizika Aprili 2. Rais Sall mwenyewe alielezea mashaka juu ya uwezekano wa uchaguzi kabla ya kuondoka kwake.

Wengine wanamshutumu kwa kuchezea muda, ama kujinufaisha upande wake kwa sababu mambo yangemtatiza katika uchaguzi wa urais, au kung'ang'ania mamlaka zaidi ya Aprili 2. Wanahofia kwamba "mazungumzo" yatatumika kuchunguza upya wagombea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.