Pata taarifa kuu

Makao makuu ya chama cha mpinzani wa Chad aliyeuawa yabomolewa

Makao makuu ya chama cha mpinzani mkuu wa jeshi la serikali nchini Chad, aliyeuawa siku ya Jumatano katika shambulio la jeshi kwenye jengo hili huko N'Djamena, yanabomolewa siku ya Ijumaa, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini.

Wafuasi wa mmoja wa wagombea wa upinzani wa rais wa Senegal wakati wa maandamano huko Dakar mnamo Februari 24, 2024.
Wafuasi wa mmoja wa wagombea wa upinzani wa rais wa Senegal wakati wa maandamano huko Dakar mnamo Februari 24, 2024. © AFP / JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Jengo hilo lilikuwa na ofisi ya Chama cha Kisoshalisti Bila Mipaka (PSF) cha Yaya Dillo Djérou, binamu ya Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, aliyetangazwa kuwa rais wa Jamhuri ya Mpito na utawala wa kijeshi mwaka wa 2021. Bw. Djérou aliuawa katika shambulio hilo, ambalo lilisababisha jumla ya watu saba kuuawa kulingana na serikali, askari wanne na watatu katika safu ya Bw. Dillo waliuawa.

Mashine moja kubwa imebomoa jengo hilo la ghorofa tatu, waandishi wawili wa habari wa AFP wameripoti mchana, wakiwa wamehifadhiwa kwa umbali na ngome nene ya ulinzi ya jeshi, ambapo magari ya kivita yalionekana kwa mbali yakizingira jengo hilo.

Kulingana na serikali, Bw. Dillo, ambaye aikuwa akisakwa na polisi kwa kuanzisha madai ya "jaribio la mauaji" dhidi ya Rais wa Mahakama ya Juu siku kumi zilizopita na shambulio kwenye makao makuu ya idara kuu za upelelezi siku ya Jumanne, aliuawa katika shambulio hilo "kwa sababu alikataa kujisalimisha" na "alijipiga risasi ". Hili linapingwa na PSF na upinzani, ambao wanazungumzia "mauaji" miezi miwili kabla ya uchaguzi wa rais, ambao alipaswa kugombea, dhidi ya Jenerali Déby.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.