Pata taarifa kuu

Senegal: Baada ya wiki za mzozo, uchaguzi wa urais kufanyika Machi 24

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza siku ya Jumatano kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais itafanyika Machi 24, baada ya wiki za mgogoro mkubwa na uamuzi wa Baraza la Katiba kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi baada ya mwisho wa muhula wake Aprili 2.

Senegal: Rais Macky Sall alifungua mazungumzo ya kitaifa Jumatatu Februari 26 huko Diamniadio, karibu na Dakar, ambapo viongozi wengi wa kisiasa walikataa kushiriki.
Senegal: Rais Macky Sall alifungua mazungumzo ya kitaifa Jumatatu Februari 26 huko Diamniadio, karibu na Dakar, ambapo viongozi wengi wa kisiasa walikataa kushiriki. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Jamhuri amearifu Baraza la Mawaziri kuhusu tarehe ya kifanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Jumapili Machi 24, 2024," imesema taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa na msemaji wa ofisi ya rais. Tangazo hili linafuatia kuchapishwa kwa uamuzi wa Baraza la Katiba ambalo liliamua kwamba uchaguzi wa urais ufanywe kabla ya Aprili 2, na kukataa tarehe iliyopendekezwa ya Juni 2.

"Kuweka tarehe ya uchaguzi zaidi ya muda wa muhula wa Rais wa Jamhuri madarakani ni kinyume na Katiba," unasema uamuzi wa "Wahenga" ulioandikwa siku ya Jumanne na kuthibitishwa na shirika la habari la AFP.

Baraza la Katiba pia lilikataa pendekezo lingine lililotolewa kwa Rais Sall na kutangaza kuwa orodha ya wagombea 19 ambayo tayari imethibitishwa na taasisi hiyo isifanyiwe marekebisho.

Ofisi ya rais wa Senegal imebaini uharakishaji huu wa ghafla wa kalenda kwa kutangaza jioni kwamba Waziri Mkuu Amadou Ba "ameodolewa" kwenye wadhifa wake kwa minajili ya kuongoza kampeni. Nafasi yake inachukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Sidiki Kaba, msemaji mmoja amesema.

Baraza la Katiba liliombwa tangu siku ya Jumatatu kwa maoni yake na Rais Sall mwenyewe. Mkuu huyo wa nchi aliwasilisha mapendekezo yaliyotokana na "mazungumzo ya kitaifa" ambayo aliitisha wiki iliyopita ili kujaribu kuiondoa nchi hii katika mgogoro uliosababishwa na kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais, mojawapo ya mazungumzo makubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.