Pata taarifa kuu

Senegal: Umoja wa Ulaya wapinga Rais Macky Sall kuongezwa muda wa kusalia mamalakani

Umoja wa Ulaya (EU) umekuwa ukifuatilia matukio nchini Senegal kwa umakini na wasiwasi tangu kutangazwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Senegal, Dakar (picha ya kielelezo).
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Senegal, Dakar (picha ya kielelezo). CC/Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya ulituma ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mapema Februari nchini Senegal. Sasa unabaini kwamba ahadi za Macky Sall za kutokwenda zaidi ya mwisho wa muhula wake lazima ziheshimiwe.

Nabila Massrali, msemaji wa idara ya Diplomasia ya Ulaya, akihojiwa na Pierre Benazet amesema Umoja wa Ulaya inapinga hatu yoyote ya kuongezwa muhula wa rais nchini Senegal: "Umoja wa Ulaya unarejelea uamuzi wa Baraza la Katiba la Senegal ambalo linatoa wito kwa mamlaka kuandaa uchaguzi wa urais haraka iwezekanavyo, kwa kuzingatia ukweli kwamba uchaguzi hauwezi kuahirishwa zaidi ya muhula wa mamlaka ya rais.

"Kuheshimu matakwa halali ya raia"

"Umoja wa Ulaya unakaribisha uthibitisho wa Rais Macky Sall, wa kuondoka madarakani mwishoni mwa muhula wake, Aprili 2, na pia umepokea uidhinishwaji wa Baraza la Katiba wa orodha ya wagombea wa uchaguzi wa urais. Lakini Umoja wa Ulaya unasisitiza wito wake kwa mamlaka ya Senegal kuheshimu matakwa halali ya raia na nguvu zote amilifu za taifa hilo kuhifadhi demokrasia, uhuru wa kimsingi na utawala wa sheria. Umoja wa Ulaya unatoa wito kwa maandamano yoyote kuwa ya amani. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.