Pata taarifa kuu

Guinea: Jeshi kusalia madarakani hadi 2025, kulingana na Waziri Mkuu

Waziri Mkuu mpya wa Guinea Amadou Oury Bah ametambua kwamba wanajeshi walionyakua mamlaka kwa nguvu wanapaswa kusalia madarakani angalau hadi mwaka 2025 na kuvunja ahadi yao ya kuondoka mamlakani ifikapo mwisho wa mwaka 2024.

Rais wa mpito nchini Guinea, Kanali Mamadi Doumbouya, Septemba 22, 2022.
Rais wa mpito nchini Guinea, Kanali Mamadi Doumbouya, Septemba 22, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Amadou Oury Bah, aliyeteuliwa na jeshi katika wadhifa wake mwishoni mwa mwezi wa Februari, ametaja katika mahojiano na redio ya Ufaransa RFI yaliyorushwa leo Jumanne mzozo wa kiuchumi ambao nchi hiyo inakabiliana nao, hitaji la kupunguza mivutano ya sasa ya kisiasa na kijamii na nia ya kufanya kura ya maoni ya katiba ifikapo mwisho wa mwaka.

"Kuna dharura nyingi," amesema. "Katika hali ambayo sisi ni dhaifu katika kiwango cha uchumi, katika kiwango cha kifedha, lazima tufanye kazi kuelekea utulivu, kuelekea utulivu wa kisiasa ili kuwa na uwezekano wa kuchunguza na kutekeleza hatua za kalenda kwa utulivu ," amesema. "Kwa hivyo lengo ni kumaliza hii na nadhani mwaka 2025 ni wakati mzuri wa kumaliza mchakato mzima," ameongeza.

Wanajeshi waliompindua rais wa kiraia Alpha Condé mnamo mwezi Septemba 2021 walitangaza mbele ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), chini ya shinikizo la mataifa hayo, kurudisha madaraka kwa raia waliochaguliwa ifikapo mwisho wa mwaka 2024 mwishoni mwa kile kinachojulikana kama " kipindi cha mpito. Kipindi hiki ni muhimu kulingana na wao kufanya mageuzi makubwa na kukomesha miongo kadhaa ya kutokuwa na utulivu katika nchi hii iliyotawaliwa kwa muda mrefu na tawala za kimabavu.

Waziri Mkuu amekiri "kucheleweshwa kidogo" katika utekelezaji wa kalenda. Mamlaka bado zinapaswa kufanya sensa na kuanzisha daftari la uchaguzi, amesema. "Mwishoni mwa mwaka, kura ya maoni ya katiba inapaswa kufanyika; kuanzia wakati huo na kuendelea, michakato mingine ya uchaguzi itakataliwa," ameongeza. Amedai kuwa jeshi linaloongozwa na Jenerali Mamadi Doumbouya, ambaye aliapishwa kuwa rais, linasalia madarakani. "Uongozi mkuu wa Guinea unataka Guinea kuwa nchi ya kawaida tena," amebainisha.

Guinea ni mojawapo ya nchi za Afrika Magharibi ambako jeshi limetwaa mamlaka kwa nguvu tangu mwaka 2020. Nchini Mali pia, utawala wa kijeshi umeshindwa katika ahadi yake ya ECOWAS ya kuondoka kwenye uongozi wa nchi mapema mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.