Pata taarifa kuu

EU imetoa msaada wa Dola za Marekani bilioni 8 kwa nchi ya Misri

Nairobi – Umoja wa Ulaya, umetangaza kuipa Misri kiasi cha dola za Marekani bilioni 8 kama mkopo na msaada, fedha inazotoa wakati huu nchi wanachama zikijaribu kukabiliana na wimbi la wahamiaji.

Aidha EU imetangaza kutoa msaada zaidi kwa nchi hiyo kusaidia katika sekta ya nishati na ujenzi wa uchumi wake
Aidha EU imetangaza kutoa msaada zaidi kwa nchi hiyo kusaidia katika sekta ya nishati na ujenzi wa uchumi wake AFP - STAVROS IOANNIDES
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo umetajwa kuwa unaboresha zaidi uhusiano wa EU na Misri.

Misaada, mikopo na fedha zingine zinapaswa kuwasilishwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kusaidia uchumi unaodorora wa Misri.

Misri ilijitolea kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kwenda Ulaya
Misri ilijitolea kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kwenda Ulaya AFP - -

Mgogoro wa kifedha unaoendelea kushuhudiwa nchini humo umesababisha kuongezeka kwa idadi ya raia wa Misri wanaojaribu kuvuka kuelekea Ulaya, hasa kupitia Libya kutafuta maisha bora.

Ursula von der Leyen ni rais wa Kamisheni ya umoja wa Ulaya.

“Nguzo ya nne ni uhamiaji na uhamaji ambapo tayari tuna ushirikiano mzuri sana na hii inahitajika zaidi kuliko hapo awali.” alisema Ursula von der Leyen ni rais wa Kamisheni ya umoja wa Ulaya.

00:36

Ursula von der Leyen ni rais wa Kamisheni ya umoja wa Ulaya

Aidha EU imetangaza kutoa msaada zaidi kwa nchi hiyo kusaidia katika sekta ya nishati na ujenzi wa uchumi wake.

Misri ilijitolea kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kwenda Ulaya.

EU katika siku za nyuma ilitia saini mikataba sawa na nchi nyingine za bara Afrika ambazo zinatumika kama njia kwa  uhamiaji usio wa kawaida kwenda Ulaya, ikiwa ni pamoja na Tunisia, Libya na Mauritania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.