Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Libya yafunga kituo cha mpaka na Tunisia baada ya makabiliano

Libya imefunga kivuko chake kikuu cha mpaka na Tunisia siku ya Jumanne baada ya makabiliano kati ya makundi yenye silaha na vikosi vya usalama katika upande wa mpaka wa Libya, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tripoli imetangaza.

Maafisa wa idara ya Ushuru na Forodha ya Tunisia wakikagua lori kutoka Libya baada ya kuvuka hadi Tunisia kupitia mpaka wa Libya na Tunisia wa Ras Jedir, Aprili 7, 2014.
Maafisa wa idara ya Ushuru na Forodha ya Tunisia wakikagua lori kutoka Libya baada ya kuvuka hadi Tunisia kupitia mpaka wa Libya na Tunisia wa Ras Jedir, Aprili 7, 2014. © Fathi NASRI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wizara imebaini katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba imeagiza "kufungwa mara moja" kwa kituo cha mpaka cha Ras Jedir "kufuatia shambulio lililofanywa na makundi haramu" yaliyohusika haswa katika shughuli za magendo "ambazo yanachukulia kama haki waliopewa.

Kufungwa huku kunalenga kuwezesha "utekelezaji wa mipango ya usalama" na kuhakikisha utendakazi wake ufaao "chini ya mamlaka ya Serikali", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

"Hatutavumilia tena machafuko haya" huko Ras Jedir, wizara imeonya, na kuongeza kuwa makundi "haramu", ambayo haikubaini, "yatashitakiwa na kuadhibiwa vikali". Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Imad Trabelsi, aliagiza "Kikosi cha Utekelezaji Sheria", kilicho chini ya mamlaka ya wizara yake, kuingilia kati Ras Jedir ili "kupambana na magendo na unyanyasaji" na kuhakikisha usalama wa wasafiri.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, makabiliano yalizuka siku ya Jumatatu kati ya makundi ambayo kwa hakika yalikuwa yakidhibiti kituo hiki cha mpaka na vikosi vya usalama vilivyotumwa na Tripoli. Ras Jedir ambayo inapatikana kaskazini-magharibi mwa Libya, kilomita 170 magharibi mwa Tripoli, ni kivuko kikuu kati ya magharibi mwa Libya na kusini mashariki mwa Tunisia, eneo ambalo hutumiwa kwa sehemu kubwa ya biashara ya mipakani, ikiwa ni pamoja na magendo.

Makundi kutoka miji ya Libya katika eneo hilo kwa miaka mingi yamedhibiti kituo cha mpaka ambacho wanakichukulia kuwa hifadhi yao ya kibinafsi, ambayo iko katika eneo lao na ambayo inawaruhusu kufanya biashara isiyo rasmi yenye faida kubwa sana.

Kufungwa kwa kituo hiki kunatatiza upitishaji wa bidhaa katika pande zote mbili lakini pia wafanyakazi wengi wa Tunisia wanaofanya kazi nchini Libya na Walibya wanaokwenda Tunisia, haswa kutafuta matibabu kushindwa kupita katika kituo hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.