Pata taarifa kuu

Libya: Amnesty yataka uchunguzi ufanyike kuhusu wahusika wa janga la Derna,

Miezi sita iliyopita, mji wa Derna, nchini Libya, ulivamiwa na maji baada ya mabwawa mawili kuvunjika, hali iliyosababishwa na kimbunga cha Storm Daniel. Matokeo: zaidi ya watu 4,300 walifariki dunia, maelfu kupotea na karibu 45,000 kuhama makazi yao.

Moja ya maeneo ya mji wa Derna, Libya, ulioharibiwa na mafuriko.
Moja ya maeneo ya mji wa Derna, Libya, ulioharibiwa na mafuriko. © Jamal Alkomaty / AP
Matangazo ya kibiashara

Leo Jumatatu, Machi 11, 2024, shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International linatoa ripoti kuhusu maafa haya ambapo inashutumu ukosefu wa haki katika upatikanaji wa fidia na kutoa wito wa uchunguzi wa kina kuhusu wajibu wa watendaji wenye nguvu wa kijeshi na kisiasa.

Ni shtaka la kweli dhidi ya serikali ya umoja wa kitaifa na vikosi vya kijeshi vya Waarabu wa Libya ambao sirika hili lisilo la kiserikali linashi=ushia lawama katika ripoti hii. Amnesty International kwanza inashutumu kutotosheleza kwa maonyo na maagizo yanayopingana yaliyotolewa na mamlaka kabla ya kupita kwa kimbunga cha Storm Daniel.

“Baadhi ya maofisa wa ngazi za juu, akiwemo mkurugenzi wa usalama, wamewataka wananchi kuheshimu kikamilifu itifaki ya tahadhari inayotumika jijini, huku katika maeneo mengine, mamlaka imetoa wito kwa wakazi kuhama. Kwa hivyo watu walipotea kweli,” anasema Bassam al-Kantar, mtafiti wa Amnesty nchini Libya. Na akaongeza: "Na wale waliohama maeneo ya karibu na bahari walihamia sehemu ambazo ziliathiriwa zaidi."

Ingawa watu 13,000 walioathiriwa na maafa walilipwa fidia, Amnesty inanyooshea kidole ukosefu wa haki katika kupata misaada na fidia za kifedha. Baadhi ya familia zilizohama makazi yao, wakimbizi na wahamiaji, wametengwa. "Hawakuwahi kupokea fidia yoyote," analalamika Bw. al-Kantar.

“Serikali ya mashariki imesema iliunda kamati wiki mbili baada ya maafa ili kuruhusu tathmini kamili ya wageni walioathiriwa na mafuriko. Lakini miezi 5 baada ya kuundwa kwa kamati hii, hakuna kilichofanyika,” anaongeza.

Haiwezekani leo, kulingana na Amnesty, kufanya ukosoaji mdogo wa namna ambayo mamlaka ilisimamia janga hilo. Wakati huo huo, Amnesty inashutumu kutokuwepo kwa uchunguzi wa majukumu ya watumishi wa umma, makamanda wa ngazi za juu na wanachama wa makundi yenye nguvu yenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.