Pata taarifa kuu

Sudan inakabiliwa na janga baya zaidi la kibinadamu kutokana na mapigano

Nairobi – Baada ya takriban mwaka mmoja wa vita, Sudan inakabiliwa na moja ya janga baya zaidi la kibinadamu katika historia ya hivi karibuni, Umoja wa Mataifa umesema hapo jana, ukishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuchukua hatua.

Mamilioni ya raia wa Sudan wanaishi katika kambi za wakimbizi ambapo wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na maji.
Mamilioni ya raia wa Sudan wanaishi katika kambi za wakimbizi ambapo wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na maji. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa operesheni za kibinadamu Edem Wosornu, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, tayari theluthi moja ya wakazi wa Sudan wanakabiliwa na uhaba wa chakula, janga la njaa likitarajiwa kwenye jimbo la darfur.

Aidha aliongeza kuwa, tathmini ya hivi majuzi ilifichua mtoto mmoja anakufa kila baada ya saa mbili katika kambi ya Zamzam huko El Fasher, Darfur Kaskazini, na kwamba washirika wao wa kibinadamu wanakadiria katika wiki zijazo, watoto zaidi ya laki mbili, wanaweza kufa kutokana na utapiamlo.

Sudan ilitumbukia katika machafuko mwezi Aprili mwaka jana, kati ya kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah Burhan na naibu wake kiongozi wa kundi la RSF Mohammed Hamdan Dagalo.

Pande hasimu za kijeshi zimeonekana kutupilia mbali wito wa jamii ya kimataifa wa kusitisha mapigano yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.