Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mali: Watoto zaidi ya kumi wauawa na shambulio la ndege zisizo na rubani za jeshi

Nchini Mali, shambulio la ndege zisizo na rubani za jeshi la Mali liliua watoto zaidi ya kumi usiku wa Jumamosi Machi 23 kuamkia Jumapili Machi 24. Hii ilitokea katika kijiji cha Douna, wilaya ya Mondoro, mkoa wa Douentza, si mbali na mpaka na Burkina Faso. Kulingana na vyanzo vya ndani vilivyohojiwa na RFI, shule ya Quran ambayo ililengwa .

Mondoro, nchini Mali.
Mondoro, nchini Mali. © Studio FMM
Matangazo ya kibiashara

Watu kumi na wanne waliuawa, haswa watoto wa kabila la Dogon: kulingana na vyanzo kadhaa vya kiraia, watu mashuhuri na wawakilishi wa kijamii, shambulio hili la ndege zisizo na rubani lilitokea karibu saa nne usiku. Kijadi, katika sehemu hii ya Mali, wanafunzi wa shule za Quran husoma mapema sana asubuhi, na jioni sana, karibu na moto. Hapo ndipo ndege isiyo na rubani ilirusha mabonu.

Picha zilizopokelewa na RFI ni ngumu kuangalia: zinaonyesha miili ya watoto iliyoharibika vibaya, iliyojaa damu... Majeruhi tisa waliripotiwa kuhamishwa hadi hospitali ya Mopti-Sévaré.

"Makosa haya lazima yakome!"  Maoni haya sio ya mwanakijiji kutoka Douna lakini ya chanzo cha usalama cha Mali, aliyehojiwa naye huko Bamako, ambaye anathibitisha mkasa huu mwingine na anahakikishia kwamba " watu wamepaza sauti ", ikiwa ni pamoja na ndani ya vikosi vya usalama vya Mali, dhidi ya makosa haya ya mara kwa mara wakati wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Wiki moja tu iliyopita, raia 14, wakiwemo wanawake na watoto, waliuawa huko Amasrakad, mkoa wa Gao.

Wakati huo huo, mashambulizi mengine yalifanywa kaskazini mwa Mali. Vyanzo vingine vinahakikisha kwamba raia waliuawa, habari ambazo RFI haikuweza kuthibitisha rasmi.

Kijiji cha Douna kinapatikana kusini zaidi, katikati mwa Mali, katika eneo ambalo wakaazi wameteseka kwa muda kwa ukatili wa wanajihadi wa Jnim, Kundi linalodai kusaidia Uislamu na Waislamu, lenye uhusiano na al-Qaeda.

Kwa ombi la RFI, jeshi la Mali halikujibu, na halikuchapisha taarifa yoyote kwa vyombo vya habari kuhusu shambulio hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.