Pata taarifa kuu

Sudan: Mamilioni ya watu wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini Chad

Takriban watu milioni 3 na laki 4 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu nchini Chad, kutokana na kuendelea kuwasili kwa idadi kubwa ya wakimbizi wa Sudan wanaokimbia vita, shirika lisilo la kiserikali la Ufaransa “Action Contre La Faim” limeonya.

Watu wa Sudan waliokimbia vita katika jimbo la Darfur nchini Sudan na hapo awali walikuwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan, wakitazama wakiwa wamesimama karibu na makazi ya muda kwenye mpaka kati ya Sudan na Chad, wakati wakikimbilia Borota, Chad. May 13, 2023
Watu wa Sudan waliokimbia vita katika jimbo la Darfur nchini Sudan na hapo awali walikuwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan, wakitazama wakiwa wamesimama karibu na makazi ya muda kwenye mpaka kati ya Sudan na Chad, wakati wakikimbilia Borota, Chad. May 13, 2023 © REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Machi mwaka huu umoja wa Mataifa ulionya kuwa, msaada wa chakula kuokoa maisha ya mamia kwa maelfu ya watu wanaotoka Sudan kukimbia vita ungekwama mwezi Aprili bila ufadhili wa kimataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liliomba msaada wa dola za Marekani milioni 242 ili kuepusha maafa na kuendelea kusaidia wakimbizi milioni 1 na laki 2 wa Sudan, wakati huu pia msimu wa mvua unaokaribia ukitishia kuharibu barabara za mashariki mwa Chad.

Taifa hilo la Afrika ya Kati, tayari lilikuwa mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani likiwa na watu milioni 1 na laki 4 waliokimbia makazi yao ndani au kutoka nchi nyingine jirani.

Vita inayoendelea Sudan, imesababisha watu milioni nane kukimbilia Chad, ambako wakimbizi wengine laki 4 tayari walikuwa wamekimbilia huko kati ya 2003 na 2020, kulingana na takwimu za UN.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.