Pata taarifa kuu

Sudan: Ni mwaka mmoja sasa tangu kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi na RSF

Leo ni mwaka mmoja kamili tangu kuanza kwa vita nchini Sudan, kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa vikosi vya RSF, mgogoro ambao umesababisha vifo vya maelfu ya raia na mamilioni kukimbilia katika nchi jirani kama Chad na Sudan Kusini.

Wanaume wamekaa nje ya tawi la benki iliyoungua kusini mwa Khartoum, Mei 24, 2023, huku kukiwa na mzozo unaoendelea Sudan kati ya jeshi na wanamgambo. Mwaka mmoja baada ya majenerali wapinzani wa Sudan kuingia katika vita hivyo, na kuitumbukiza nchi hiyo katika dhoruba ya watu wengi kuhama makwao, njaa, ukatili wa kingono na kikabila, wataalam hawaoni mwisho. Kulingana na Umoja wa Mataifa, nchi hiyo - ambayo tayari ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani - inakabiliwa na "moja ya majanga makubwa zaidi.
Wanaume wamekaa nje ya tawi la benki iliyoungua kusini mwa Khartoum, Mei 24, 2023, huku kukiwa na mzozo unaoendelea Sudan kati ya jeshi na wanamgambo. Mwaka mmoja baada ya majenerali wapinzani wa Sudan kuingia katika vita hivyo, na kuitumbukiza nchi hiyo katika dhoruba ya watu wengi kuhama makwao, njaa, ukatili wa kingono na kikabila, wataalam hawaoni mwisho. Kulingana na Umoja wa Mataifa, nchi hiyo - ambayo tayari ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani - inakabiliwa na "moja ya majanga makubwa zaidi. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa raia wengi wa Sudan, wanataka kuona vita hii ikikoma kama anavyoeleza hapa, Ahmed Awad, mwanafunzi wa utabibu katika chuo kikuu cha Khartoum, aliyelazimika kukiùbia Sudan Kusini.

‘‘Huu ndio ujumbe wangu, lazima vita vikomeshwe, mimi sikuwa natarajia kuwa mkimbizi, tatizo kubwa tunalokabiliwa nalo ni kupata ajira.’’ alisema Ahmed Awad, mwanafunzi wa utabibu katika chuo kikuu cha Khartoum.

00:10

Ahmed Awad, mwanafunzi wa utabibu katika chuo kikuu cha Khartoum

Kwa upande Wake, Ali Alhaji Dafalah, mjumbe wa jenerali Burhan, amesisitiza kuwa kiongozi wao yuko tayari kutoa msamaha kwa wapiganaji wa RSF ikiwa watajisalimisha.

‘‘Iwapo waasi hawa wenye silaha watakomesha uasi, tutawasamehe na tuko tayari kumkaribisha kwenye jeshi letu.’’ alieleza Ali Alhaji Dafalah, mjumbe wa jenerali Burhan.

00:14

Ali Alhaji Dafalah, mjumbe wa jenerali Burhan

Aidha kundi la RSF kupitia kwa msemaji wake, Youssif Ezzat, amesisitiza utayari wao wa kuheshimu mkataba wa usitishaji mapigano anaodai unakiukwa na jeshi kila mara.

‘‘Tunajaribu kutafakari kuhusu kusitishwa kwa mapigano, matakwa ya watu wetu ni kwamba wanataka wawe katika uongozi wa Sudan na wanataka watambuliwe rasimi kama wananchi halisi wa Sudan.’’ Youssif Ezzat,msemaji wa RSF.

00:14

Youssif Ezzat-Msemaji wa RSF

Mapigano yameendelea kuripotiwa licha ya juhudi za jumuiya ya IGAD na nchi ya Saudi Arabia na Marekani, ambazo zinajandaa kujaribu kuandaa mkutano mwingine kujaribu kuzipatanisha pande hizo mbili mjini Jeddah.

Soma piaUN yaonya kuhusu madhara ya vita vinavyoendelea nchini Sudan

James Shimanyu-Nairobi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.