Pata taarifa kuu

UN yatoa wito wa kuvunjwa kwa mitandao ya ulanguzi wa madawa ya kulevya katika Sahel

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inataka hatua za "haraka" zichukuliwe ili kukomesha mitandao ya ulanguzi wa dawa za kulevya ambayo inachochea kukosekana kwa utulivu katika nchi za Sahel, katika ripoti yake ya mwaka 2024 iliyochapishwa siku ya Ijumaa.

Afisa wa polisi akimwaga petroli kwenye tani 4 za dawa za kulevya ambazo ziliteketezwa katika Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Utumiaji Mbaya na Usafirishaji wa Dawa za Kulevya huko Conakry, Guinea, Juni 26, 2013.
Afisa wa polisi akimwaga petroli kwenye tani 4 za dawa za kulevya ambazo ziliteketezwa katika Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Utumiaji Mbaya na Usafirishaji wa Dawa za Kulevya huko Conakry, Guinea, Juni 26, 2013. © Cellou Binani / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Nchi za Sahel na jumuiya ya kimataifa lazima zichukue hatua za haraka, zilizoratibiwa na za kina ili kukomesha mitandao ya ulanguzi wa dawa za kulevya", iliyoanzishwa vyema ndani ya Mataifa na wasomi wa ndani, anaonya Leonardo Santos Simão, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika Magharibi na Sahel,  aliyenukuliwa katika ripoti hii.

Nchini Mali, Burkina Faso na Niger, nchi tatu zinazoongozwa na tawala za kijeshi ambapo makundi yenye silaha, hasa wanajihadi, hudhibiti maeneo makubwa katka nchi hizo, "utawala dhaifu wa sheria unawezesha upanuzi wa uchumi wa madawa ya kulevya, ambao unaweza, kwa upande wake, kutoa rasilimali za kifedha ili kudumisha au kuzidisha migogoro", inabainisha UNODC.

Nchi hizi zilizo na mipaka yenye upenyo ni njia za kupitisha dawa zinazotoka bandarini katika nchi za Ghuba ya Guinea hadi Bahari ya Mediterania na Ulaya, kupitia njia za Sahara.

"Wafanyabiashara walitumia mapato yao kupenya tabaka tofauti za serikali" kupitia rushwa, inasema UNODC.

Ulanguzi wa dawa za kulevya "unawezeshwa na watu mbalimbali, wakiwemo wasomi wa kisiasa, viongozi wa jumuiya na viongozi wa makundi yenye silaha" na unawezesha makundi haya yenye silaha "kudumisha ushiriki wao katika vita, hasa kupitia ununuzi wa silaha", kulingana na waandishi wa ripoti hii.

Katika miaka ya hivi karibuni, ukanda huo pia umekuwa eneo la matumizi. Resin ya bangi inasalia kuwa dawa inayokamatwa mara kwa mara katika nchi za Sahel, ikifuatiwa na kokeini na opioids.

Kiasi cha kokeini iliyonaswa katika Sahel iliongezeka sana mwaka wa 2022. Makundi ya wahalifu wenye silaha, wanaotaka kujitenga, wanajihadi au washirika wa serikali zilizopo wanahusika kwa viwango tofauti katika usafirishaji huu, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.