Pata taarifa kuu

Niger : Raia wameandamana kushinikiza kuondoka wa wanajehsi wa Marekani

Nchini Niger, kumekuwa na maandamano ya raia wa jimbo la Agadez kushinikiza kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani katika eneo lao.

Raia wa Niger akiwa ameshikilia bango la kuwataka wanajeshi wa Jeshi la Marekani kuondoka Niger wakati wa maandamano huko Niamey, tarehe 13 Aprili 2024.
Raia wa Niger akiwa ameshikilia bango la kuwataka wanajeshi wa Jeshi la Marekani kuondoka Niger wakati wa maandamano huko Niamey, tarehe 13 Aprili 2024. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya serikali ya Marekani siku ya Ijumaa kukubali kuondoa wanajeshi wake zaidi ya Elfu Moja, katika nchi hiyo, inayoongozwa na wanajeshi kwa sasa.

Hii ilitanguliwa na uongozi wa Niger, kutangaza kusitisha mara moja, ushirikiano wa kijeshi na Marekani, hatua ambayo pia imeungwa mkono na mashirika ya kiraia nchini humo.

Soma piaMarekani yakubali kuondoa kikosi chake cha kupambana na wajihadi Niger

Tangazo la Marekani kukubali kuondoa vikosi vyake ambavyo vimekuwepo nchini humo tangu mwaka 2013, kusaidia kupambana na makundi yenye silaha, inaonekana kama ushindi kwa Agadez êneo ambalo limekuwa ngome ya wanajeshi háo, ambao kwa wiki kadhaa sasa wamekuwa wakipata shinikizo ya kuondoka.

Maktaba: Bendera za Marekani na Niger katika kambi ya wanajeshi wa anga na wafanyakazi wengine wanaosaidia ujenzi wa kituo cha ndege cha Niger Air Base 201 huko Agadez, Niger, Aprili 16, 2018.  (AP Photo/Carley Petesch, File)
Maktaba: Bendera za Marekani na Niger katika kambi ya wanajeshi wa anga na wafanyakazi wengine wanaosaidia ujenzi wa kituo cha ndege cha Niger Air Base 201 huko Agadez, Niger, Aprili 16, 2018. (AP Photo/Carley Petesch, File) AP - Carley Petesch

Wachambuzi wa mambo wanasema, hatua hiyo ya Marekani huenda ikaifaa Urusi ambayo imekuwa ikituma kikosi chake cha Wagner katika ukanda huo, katika nchi za Mali na Burkina Faso ambazo pia zinaongozwa na jeshi.

Douglas Omariba- RFI-Kiswahili Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.