Pata taarifa kuu
ISRAEL -PALESTINA

Mashambulizi mapya ya Israel huko Gaza yaua watu 11

Mashambulizi mapya ya angani yanayofanywa na Israel kwenye ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya watu 11mapema leo Jumamosi, wakati kampeni hiyo ya kuzuia mashambulizi ya roket kutoka kwa kundi la Hamas ikiingia siku yake ya 12 huku idadi ya wapalestina waliouawa ikifikia 307 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Askari wa Israel wakiwa kwenye vifaru wakitaka kuvuka mpaka kati ya Israel na Gaza,
Askari wa Israel wakiwa kwenye vifaru wakitaka kuvuka mpaka kati ya Israel na Gaza, REUTERS/ Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo mampya yanajiri wakati huu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akielekea kwenye ukanda huo kusaidia juhudi za kusitisha mapigano huku Israel ikisema kuwa inajiandaa kuongeza operesheni ya ardhini kwenye ukanda huo.

Rais wa Marekani Barack Obama ameiunga mkono Israel akisema kuwa ina haki kujilinda dhidi ya mashambulizi ya roketi,lakini ameitaka kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka vifo vya watu wasio na hatia katika operesheni hiyo.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, hapo jana alitangaza kuanza rasmi kwa operesheni za ardhini za majeshi yake kwenye eneo la ukanda wa Gaza wakitafuta mashimo ambayo yamekuwa yakitumiwa na wapiganaji hao kupenya na kuingia Israel kufanya mashambulizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.