Pata taarifa kuu
IRAQ-UN-ISIL-Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha pendekezo kuhusu kudhibiti makundi ya kiislam nchini Iraq

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kauli moja jana Ijumaa limepitisha azimio linalolenga kudhoofisha makundi ya Kiislam nchini Iraq huku kukiwa na kuwa wanajihadi wa IS wamewaua wakazi kadhaa wa maeneo ya Yazidi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano uliopitisha pendekezo kuhusu kudhibiti makundi ya kiislam nchini Iraq  15 Agost 2014
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano uliopitisha pendekezo kuhusu kudhibiti makundi ya kiislam nchini Iraq 15 Agost 2014 AFP/Don Emmert
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya Magharibi vimeripoti kuwa wanaume kadhaa kutoka imani ya Yazidi wameuawa katika kijiji cha Kocho, kilomita 45 kutoka mji wa Kikurdi unaoshikiliwa wa Sinjar.

Baadhi ya ripoti zinasema wakazi hao waliambiwa wabadilishe dini na kuwa waislamu la sivyo wanyongwe.

Wakati taarifa zaidi kuhusu tukio hilo la hivi majuzi zikiwa hazijathibitishwa mara moja, mashambulizi hayo katika siku za nyuma yalisababisha jeshi la Marekani kuchukua hatua.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema wiki ya kwanza ya mashambulizi ya anga yamevunja eneo la mateka kaskazini mwa mlima Sinjar ambapo raia wanajificha kwa zaidi ya siku 10 wakiogo[a mashambulizi ya wanajihadi.

Marekani imefanya mashambulizi zaidi ya anga jana Ijumaa jeshi limesema, baada ya kupokea taarifa kuwa wanajihadi wa IS wamewashambulia raia katika eneo hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.