Pata taarifa kuu
IRAQ-UFARANSA-EU-Usalama

Iraq : mkutano kuhusu uwezekano wa kuwapa silaha wakurdi wafanyika Brussels

Mabalozi 28 wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels kujadili kuhusu machafuko yanayoendelea nchini Iraq.  

Ufaransa ikiwapa msaada wa kibinadamu raia wa Iraq waliyohama makaazi yao kufuatia mapigano.
Ufaransa ikiwapa msaada wa kibinadamu raia wa Iraq waliyohama makaazi yao kufuatia mapigano. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo la Ufaransa la kuwapa silaha wakurdi na uwezekano wa kuweka eneo ambako ndege za mataifa hayo ya Umoja wa Ulaya zitakua zikidondosha msaada wa kibinadamu, ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika mkutano huo

Kuhusu suala la kuwapa silaha wakurdi nchini Iraq, Ufaransa inaweza ikapata uungwaji mkono wa mataifa yenye nguvu ya kijeshi barani Ulaya, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Uhispania au Italia. Mataifa mengine, ambayo ni Ujerumani, Sweden na Austria, yamekata kutuma silaha kwa taifa linalokabiliwa na vita. Hata katika machafuko yanayoendelea nchini Syria, Austria haikukubaliana na suala la kuwapa silaha waasi wanaopigana dhidi ya utawala wa Bashar Al Assad.

Wataalamu wa masuala ya ulinzi wamebaini kwamba itakua vigumu kwa Umoja wa Ulaya kutuma silaha kwa nchi iliyowekewa vikwazo vya silaha na jumuiya ya kimataifa.

Hata hivo, si serikali ya Iraq itakayopewa silaha hizo, bali ni namna ya kusaidi wakurdi kujihami dhidi ya wanamgambo wa kislamu wanaoshikilia baadhi ya maeno ya Iraq. Kuna wasiwasi pia kwa wakurdi iwapo watapewa silaha, kunauwezekano wa kujitenga na taifa la Iraq.

Kuhusu msaada wa kibinadamu, Umoja wa Ulaya huenda ukaongeza kiwango cha msaada kwa raia wa Iraq, msaada ambao utagharimu Uro milioni 12 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.