Pata taarifa kuu
IRAQ-Usalama

Iraq : takribani watu 60 wauawa katika shambulio dhidi ya basi la wafungwa

Makundi ya watu wenye silaha yameshambulia alhamisi wiki hii basi la wafungwa waliyokua wakihamishwa sehemu nyingine kaskazini mwa mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kusababisha mapigano makali kati ya wapiganaji wa makundi hayo na wanajeshi.

Wafungwa zaidi ya 50 wauawa katika shambulio mjini Baghdad, nchini Iraq, polisi na jeshi vyanyooshewa kidole.
Wafungwa zaidi ya 50 wauawa katika shambulio mjini Baghdad, nchini Iraq, polisi na jeshi vyanyooshewa kidole. REUTERS/Ahmed Saad
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 60, vyanzo vya polisi vimefahamisha.

“Takribani watu 60, wakiwemo wafungwa na askari polisi, wameuawa katika shambulio la kuvizia, ambalo limefuatiwa na miripuko, huku risase zikifyatuliwa, afisa wa wizara ya mambo ya ndani ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Afisa huyo amebaini kwamba shambulio hilo limelenga msafara wa magari ya polisi yaliyokua yakilinda basi la wafungwa zaidi ya sitini, ambao wamekua wakihamishwa sehemu nyingine. Idadi kubwa ya wafungwa hao wanakabiliwa na tuhuma za ugaidi na wamekua wakizuiliwa katika jela kuu ya Taji, kilomita 25 kaskazini mwa Baghdad.

Vyanzo vya kiusalama vimebaini kwamba takribani wafungwa 50 wameuawa, huku vikijiuliza ni katika mazingira gani kwa muda mfupi kama huo watu hao wameuawa.

Shambulio hili linatokea muda mfupi kabla ya mkutano kati ya katibu mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moo na waziri mkuu wa Iraq, Nouri Al Malik katika jitihada za pamoja ili kushawishi jumuiya ya kimataifa dhidi ya mashambulizi yaliyoanzishwa na makundi ya waislamu wenye itikadi kali.

Shambulio hilo linatokea mwaka moja baada ya mashambulizi yaliyoendeshwa na makundi ya wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali dhidi ya jela mbili (taji na lile la Abou Ghraib), ambayo yalisababisha vifo vya askari polisi 20

Wafungwa 500 wa jela kuu la Abou Ghraib walifaulu kutoroka kufuatia mashambulizi hayo dhidi ya magari ya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.