Pata taarifa kuu
IRAQ-SYRIA-Usalama-Siasa

ISIL yamtangaza Abu Bakr al-Baghdadi kuwa khalifa katika maeneo yanayoshikiliwa

Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa ISIL wanaopigana nchini Iraq na Syria hapo jana jioni wametangaza kuanzisha utawala wa kiislamu kwenye maeneo ambayo wanayashikilia kwenye mataifa hayo.

Rekodi ya Abou Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa eneo la kislam kwenye mtandao wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.
Rekodi ya Abou Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa eneo la kislam kwenye mtandao wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani. REUTERS/Rewards For Justice
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake iliyotolewa kwa njia ya Redio, kundi hilo limemtangaza Abu Bakr al-Baghdadi kuwa mtawala wa kiislamu atakayesimamia shughuli za mataifa yote mawili na hasa kwenye maeneo ambayo wanayashikilia kwa sasa.

Kundi hilo limewataka wananchi kwenye mji wa Allepo kaskazini mwa Syria, Diyala katikati mwa nchi ya Iraq kuheshimu utawala mpya ambao umetangazwa na kwamba sharia ndio itakayokuwa ikitumika kutawala maeneo hayo.

Tangazo hili limezidisha hofu miongoni mwa mataifa ya magharibi ambayo yamekuwa yakilipiga vita kundi la ISIL lenye uhusiano wa karibu na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda yakidai kuwa kuendelea kusambaa kwa itikadi za kundi hilo kunahatarisha usalama wao na eneo zima la mashariki ya kati.

Magari ya jeshi la Iraq yakichomwa moto, katika mji wa Mossoul,baada ya kudhibitiwa na wapiganaji wa kislam wa ISIL.
Magari ya jeshi la Iraq yakichomwa moto, katika mji wa Mossoul,baada ya kudhibitiwa na wapiganaji wa kislam wa ISIL. REUTERS/Stringer

Baghdadi anakuwa kiongozi wa juu wa kidini kutangazwa na kundi hilo ambalo linasisitiza kuwa atakuwa kama shujaa wa atakayesimamia vita dhidi ya uvamizi wa mataifa ya magharibi kwenye ardhi ya waislamu.

Katika uwanja wa mapigano nchini Iraq, jeshi linaendelea na masham,bulizi ili kujaribu kuuweka mji wa Tikrit na miji mingine inayoshikiliwa na wapiganaji wa kiislamu wa kundi la ISIL katika himaya yake. Mashambulizi hayo yalianzishwa kabambe yalianzishwa juni 9 mwaka huu.

Utawala wa ukhalifa ulianzishwa katika ulimwengu wa kislam baada ya kifo cha mtume Muhamad, kama “amir wa wa waaminifu”, lakini utawala huo ulipotea baada ya utawala wa Othman.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kutokana na machafuko hayo yanayoendelea nchini Iraq, ambapo maelfu ya raia wameuawa na wengine mamia kwa maelfu wameyahama makaazi yao kutokana na machafuko hayo, amesema msemaji wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.