Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-ISIL-Usalama

Iraq: ISIS yakabiliwa na mashambulizi ya Marekani

Marekani imeanza mashambulizi mapya dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa ISIS nchini Iraq katika miji ya Mosul Dam na Amerli.

Wakaazi wa Mosul Dam wakiyakimbia makaazi yao kufuatia mapigano yanayoendela kati ya wanajeshi wa Iraqyakishirikiana na wapiganaji wa Kikurdi kwa usaidizi wa jeshi la Marekani dhidi ya wapiganaji wa kiislam.
Wakaazi wa Mosul Dam wakiyakimbia makaazi yao kufuatia mapigano yanayoendela kati ya wanajeshi wa Iraqyakishirikiana na wapiganaji wa Kikurdi kwa usaidizi wa jeshi la Marekani dhidi ya wapiganaji wa kiislam. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon inasema ndege zake za kivita zimefanikiwa kuharibu magari ya wapiganaji wa ISIS karibu na mji wa Mosul Dam.

Licha ya kujaribu kuliangamiza kundi hili, Marekani imesema mashambulizi haya pia yamesaidia ili msaada wa kibiandamu uwafikie wanajeshi wa Iarq wanaopambana na wapiganaji hawa ambao wamejihami vilivyo.

Hadi sasa Marekani imetekeleza mashambulizi ya anga 120 dhidi ya wapiganaji wa kiislam ambao imesema ni hatari na haijawahi kuona kundi lililojihami kwa silaha hatari kama ISIS.

Makabiliano haya pia yamesabisha raia wengi kukimbia makwao na wakaazi wa Amerli hawana chakula na wale wanahofia maisha yao kwa kile wanachodai ni Washia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.