Pata taarifa kuu
MAREKANI-FERGUSON-MAANDAMANO-Usalama

Kifo cha Brown: vurugu zatokea katika mji wa Ferguson

Jupo la wanasheria limeamua kutomfungulia mashitaka askari polisi aliyehusika katika kifo cha kijana mweusi raia wa Marekani, Michael Brown mwezi Agosti. Askari polisi huyo alimuua Michael Brown kwa kumpiga risase sita katika mji wa Ferguson, katika jimbo la Missouri.

Vurugu zatokea katika mji wa Ferguson katika jimbo la Missouri, baada ya uamzi wa jopu la wanasheria wa kutomfungulia mashitaka askari polisi aliyemuua Michael Brown.
Vurugu zatokea katika mji wa Ferguson katika jimbo la Missouri, baada ya uamzi wa jopu la wanasheria wa kutomfungulia mashitaka askari polisi aliyemuua Michael Brown. REUTERS/Jim Young
Matangazo ya kibiashara

Raia wa mji wa Ferguson wameghadhabishwa na uamzi huo uliyotolewa na jopu la wanasheria.

Maelfu ya raia ambao walikua mbele ya kituo cha polisi cha mji wa Ferguson, walimsikia kwa simu mwendesha mashitaka wa eneo la St Louis akieleza kwa nini jopu la wanasheria limechukua uamzi wa kutmfungulia mashitaka askari polisi aliyemuua Michael Brown.

"Wajibu wa jopu la wanasheria ni kutenganisha tukio kutoka na uongo," amesema mwendesha mashitaka, Robert McCulloch, mbele ya vyombo vya habari.

Michael Brown, mwenye umri wa miaka 18, ambaye hakua na silaha, aliuawa mchana kweupe akipigwa risasi sita mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka 2014. Tukio hilo lilizua machafuko ambayo yamekua yakiendelea katika mji wa Ferguson katika jimbo la Missouri.

Baada ya kusikia uamzi huo wa jopu la wanasheria, wakaazi wa mji wa Ferguson, ambao walikua wamekusanyika nje ya kituo cha polisi walipigwa na mshangao kwa muda wa sekunde thelathini, kabla ya ghadhabu kuzuka, ameweza kushuhudia mwanahabari wa RFI aliyetumwa katika mji wa Ferguson, Anne-Mary Capomaccio. Mama Michael Brown alikuwepo, akisimama juu ya gari, huku machozi yakimtiririka. Mama wa Brown ametoa wito kwa utulivu na baadae kaporomoka kutoka juu ya gari hadi sakafuni.

Wakati huohuo waandamanaji waliingia barabarani na kuanza kukabiliana na polisi, huku wakisema: " demokrasia inaendana na sheria". Waandamanaji hao waliirushia poilisi mawe, simu zao na mabango waliyokua wakibeba.

Hata hivo rais wa Marekani Barack Obama, amewatolea wito raia wa mji wa Ferguson hasa waandamanaji kuwa watulivu na kukubaliana na uamzi wa jopu la wanasheria, huku akiwataka polisi kujizuia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.