Marekani: Baadhi ya miji yakumbwa na machafuko
Zaidi ya wanajeshi elfu 2 wamepelekwa kwenye mji wa Ferguson nchini Marekani ambako maelfu ya raia wanaandamana kupinga uamuzi wa jupu la wanasheria kwenye mahakama mjini humo.
Imechapishwa:
Waandamanaji hao wamelituhumu jopu hilo kushindwa kumfungulia kesi polisi anayedaiwa kumuua Michael Brown kijana mwenye asili ya kiafrika.
Mamia ya wananchi wameendelea kukabiliana na polisi kwenye mji huo pamoja na miji mingine ya marekani wakipinga uamuzi huu wanaodai umekwenda kinyume na matakwa ya sheria, huku wanaharakati wa kutetea haki za binadamu akiwemo mwanaharakati mkongwe Al Sharpton wakilaani uamuzi uliotolewa kuhusu kesi hii.
Kwa upande wake mwanasheria wa familia ya Michael Brown, Benjamin Crump, amesema kuwa uamuzi huu haukuzingatia haki licha ya ushahidi wa kutosha aliouwasilisha kwa jupo hilo la wanasheria.
Rais Barack Obama ameendelea kutoa wito kwa wakaazi wa mji wa Ferguson kujiepusha na vurugu ikiwemo kuchoma moto magari na kufanya vitendo vya uporaji akiahidi kuwa watu waliohusika na vurugu hizo watachukuliwa hatua za kisheria.