Pata taarifa kuu
MAREKANI-CIA-AFGHANISTAN-IRAQ-HAKI

Ripoti ya CIA kuhusu mateso yatazamiwa kutolewa

Baraza la Seneti nchini Marekani linatazamiwa kutoa ripoti Jumanne Desemba 9 kuhusu mateso yaliyotekelezwa katika jela za siri za CIA wakati wa vita nchini Iraq na Afghanistan.

Alama ya CIA kwenye makao makuu ya Idara ya ujasusi y Marekani katika mji aw Langley, Virginia.
Alama ya CIA kwenye makao makuu ya Idara ya ujasusi y Marekani katika mji aw Langley, Virginia. AFP PHOTO/SAUL LOEB/FILES
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imelani mateso yalityofanyiwa mahabusu katika jela za Idara ya ujasusi ya Marekani kati ya mwaka 2002 na 2009.

Mfumo ambao Barack Obama alikomesha wakati alipoingia madarakani. Ripoti hii ilicheleweshwa kwa sababu ya ubishi uliyokua ukijitokeza mara kwa mara kwenye baraza la seneti.

Usalama umeimarishwa katika idara mbalimbali za serikali ya Marekani na kwingineko duniani hasa balozi zake , wakati huu baraza la Senate likijiandaa kutoa ripoti kuonesha namna maafisa wa CIA walivyowatesa washukiwa mbalimbali wakati wa uongozi wa rais George W Bush.

Ripoti hiyo yenye kurasa 480 itatolewa leo Jumanne Desema 9 na kumekuwa na hofu kuwa inaweza kusababisha machafuko nchini Marekani.

Kikubwa katika ripoti hii ni kutoa ukweli kuhusu kampeni ya maafisa hao wa CIA katika vita dhidi ya washukiwa wa Al Qaeda baada ya mashambulizi ya kigaidi mwaka 2001.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.