Pata taarifa kuu
ISRAELI-MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Waisraeli wachanganyikiwa juu ya hotuba ya Netanyahu

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu alipokelewa na kulihutubia Bunge la Congress Jumanne Februari 3 mwaka 2015.

Hotuba ya Benjamin Netanyahu katika Bunge la Marekani la Congress ilirushwa moja kwa moja Israeli, Jumanne, Machi 3 mwaka 2015.
Hotuba ya Benjamin Netanyahu katika Bunge la Marekani la Congress ilirushwa moja kwa moja Israeli, Jumanne, Machi 3 mwaka 2015. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Benjamin Netanyahu alikemea katika hotuba yake ndefu, makubaliano katika mazungumzo yanayoendelea na Iran juu ya nyuklia, akisema kwamba ni mpango mbaya, ambao utahatarisha dunia. Hakuna jipya katika hotuba aliyoitoa Netanyahu, iliyokua ikisubiriwa na ambayo ilirushwa kwa muda mrefu nchini Israeli.

Hotuba ya Netanyahu imekosolewa na serikali ya rais Obama ambayo kwa sasa inaendeleza mazungumzo kujaribu kufikia mwafaka kuhusu mradi huo wa Nyuklia, na duru zinasema kuwa huenda mkataba ukafikiwa mwishoni mwa mwezi huu.

Rais Barrack Obama amesema hakuna jipya aliloliona katika hotuba ya Netanyahu.

Hotuba hio ya Netanyahu ilirushwa kwenye televisheni mbalimbali nchini Marekani na nchi zingine ulimwenguni, ikiwemo Isareli.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Jerusalem, Murielle Paradon, raia mjini humo walifuata hotuba ya Waziri mkuu wa Israeli katika maeneo mbalimbali ya mji, hususan katika maduka na vibanda.

Yoav, mwenye umri wa zaidi ya miaka arobaini, ambaye alifuata hotuba hio kwenye televisheni katika duka la mikate, amesema Israeli inazungukwa na maaudui.

" Tuna maadui wengi wanaotuzunguka, ni muhimu Israeli kuwa imara na kuhakikisha kwamba hakuna silaha za kiyuklia Iran”, amesema Yoav.

Yael, mwenye asili ya Marekani, amekaribisha hotuba ya Netanyahu kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, ingawa hotuba hio inatolewa, siku kumi na tano kabla ya uchaguzi nchini Israeli, amesema Yael.

" Si amini kua amechagua muda mzuri wa kutoa hotuba hio, kwani Netanyahu ametoa hotuba hio zikisalia siku kumi na tano kabla ya uchaguzi. Bora angeliitoa baada ya uchaguzi", amesema Yael.

Uchaguzi wa Wabunge nchini Israeli unatazamiwa kufanyika Machi 17 mwaka huu. Kunasubiriwa kuona iwapo hotuba ya Netanyahu kuhusu usalama itachangia chochote kwa kupigiwa kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.