Pata taarifa kuu

Marekani yakaribishwa ushujaa wa raia wake watatu

Wamarekani wamepongezwa baada ya raia watatu wa Marekani, kuonesha ujasiri wao kwa kumkabili mtu aliyekua alijihami kwa bunduki ya rashasha na bastola ambaye lengo lake lilikua kuwaua abiria waliokua wakisafiri katika treni ya mwendo wa kasi iliyokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris.

Ushujaa wa Spencer Stone (kushoto), Anthony Sadler (katikati) na Alek Skarlatos (kulia) umekaribishwa kwa pande zote za Atlantiki.
Ushujaa wa Spencer Stone (kushoto), Anthony Sadler (katikati) na Alek Skarlatos (kulia) umekaribishwa kwa pande zote za Atlantiki. REUTERS/Files TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Watatu hao pia wanatazamiwa kupokelewa katika Ikulu ya Elysee na Francois Hollande Jumatatu Agosti 24.

Picha zao zimevunja rekodi kwenye televisheni mbalimbali ulimwenguni. Ushujaa wao ulikuwa umegonga vishwa vya habari katika magazeti yote mashirika makuu ya utangazaji. Raia hao wa Marekani ambao wamepongezwa na mataifa mbalimbali ni pamoja na Spencer Stone, mwanajeshi wa jeshi la anga la Marekani, Alek Skarlatos, mwanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Taifa katika mji wa Texas, ambaye alikua akitoka likizo nchini Afghanistan, na Anthony Sadler, mwanafunzi katika tiba ya mwili, ambao wotehao ni mashujaa wapya wa Marekani.

Marafiki hao watatu walikua katika likizo barani Ulaya, kama hawangeamua kufupiza safari yao katika dakika ya mwisho mjini Amsterdam kwa kwenda Paris, Ayoub al-Khazzani, mtu aliyekua alijihami kwa bunduki ya rashasha na bastola angelitekeleza mauaji ya makubwa.

Raia hao watatu wa Marekani wamepigiwa simu na Rais Barack Obama ambaye amekaribisha "ujasiri wao wa ajabu" na ametoa shukrani zake kwa "kitendo hicho cha kishujaa". waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amepongeza raia hao.

Itakumbukwa kuwa watu wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo liliyozimwa Ijumaa jioni Agosti 21 katika treni ya mwendo wa kasi iliokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris.

Ilikuwa saa 11:50 siku ya Ijumaa wakati mtu aliyekuwa alijihami kwa bunduki ya rashasha, bastola na kisu alipofyatua risasi katika treni ya mwendo wa kasi iliyokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris.

Kwa mujibu wa ripoti za kwanza za uchunguzi, mtuhumiwa alikabiliwa na wanajeshi wawili wa Marekani alipokua akitoka chooni ambao walimsikia akishika silaha. Lakini alikamatwa muda mfupi baada ya saa 12:00 na kikosi cha askari polisi wa Ufaransa wanaopambana dhidi ya uhalifu katika kituo cha treni cha Arras na kuwekwa chini ya ulinzi.

" Kwa mujibu wa taarifa zetu, inasadikiwa kuwa askari wawili wa Marekani walisikia kelele chooni za kitu kama bunduki ya rashasha. Inasadikiwa pia kuwa askari hao waliingilia kati kumkabili mtu huyo kabla hajaweza kutumia bunduki yake katika treni ", limeeleza gazeti la La Voix du Nord katika tovuti yake. Abiria wawili walijeruhiwa: moja alijeruhiwa vikali kwa risasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.