Pata taarifa kuu
YEMEN-Mapigano-Siasa-Usalama

Bunge lakataa kujiuzulu kwa rais

Yemen ilitumbukia katika machafuko ya kisiasa tangu Alhamisi Januari 22 baada ya kujiuzulu kwa serikali ikifuatiwa na rais.

Mpya Rais Abd Rabbo Mansour Hadi Yemen wakati wa sherehe yake ya kuapishwa katika Bunge Februari 25 2012.REUTERS / Khaled Abdullah
Mpya Rais Abd Rabbo Mansour Hadi Yemen wakati wa sherehe yake ya kuapishwa katika Bunge Februari 25 2012.REUTERS / Khaled Abdullah REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo wa kujiuzulu kwa rais umekataliwa na Bunge la nchi hiyo, wakati ambapo mji mkuu Sanaa bado unaendelea kushikiliwa na wanamgambo wa Kishia kutoka watu wa jamii Houthi.

Serikali ya Yemen , ambayo iliteuliwa miezi mitatu iliyopita, ilimuandikia raisAbd Rabbo Mansour barua ya kujiuzulu, amesema msemaji wa serikali, akitaja kwamba uamzi huo "hautarejelewa". Wakati huo huo , rais hakuchelewa kuchukua pia uamzi wa kujiuzulu, akisema kwamba Yemen imeingia katika hali ambayo hawezi kuendelea kushikilia madaraka ya uongozi wa nchi.

Uamzi huo wa rais umefutiliwa mbali na Bunge la nchi hio katika kiko cha wabunge kiliyofanyika mapema leo Ijumaa asubuhi, kwa mujibu wa kiongozi mwandamizi wa Yemen.

Waziri Mkuu Khaled Bahah, kwa upande wake, ametetea uamuzi wakeakibaini kwamba alitaka "kuwaepusha wajumbe wa serikali yake kutohusishwa katika hali inayoendelea nchini Yemen."

Waziri huyo wa zamani wa Mafuta, mwenye umri wa miaka 49, ambaye aliteuliwa Oktoba 13 mwaka 2014 ili kuunda serikali, ametaja nia yake ya kuwa kando na rais Hadi, ambaye anaonekana kuwa kizingiti cha makubaliano kyalioafikiwa na wanamgambo wa Kishia.

Wanamgambo wa Kishia ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya mji wa Sanaa, wanaomba washirikishwe katika taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi, huku wakipinga marekebisho ya Katiba ya kutaka kuigawa Yemen kwa majimbo sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.