Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-MAZUNGUMZO

Pakistan: mkutano wa kufufua mchakato wa amani Afghanistan

Islamabad inapokea Jumatatu hii, Januari 11, 2016 mkutano unaozishirikisha pande tatu ili kuzindua mchakato wa amani nchini Afghanistan. Wawakilishi kutoka China, Marekani, Pakistan na Afghanistan wanakutana ili kuandaa mpango kwa mazungumzo ya baadaye.

Kundi la Taliban linadhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35%  ya nchi ya Afghanistan.
Kundi la Taliban linadhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35% ya nchi ya Afghanistan. AFP PHOTO / Noorullah Shirzada
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unajumuisha pande nne. Pakistan kwanza. Kupitia mahusiano yake ya kihistoria na kundi la Taliban linaloendesha harakati zake nchini Afghanistan, kwa sasa ina uwezo wa kuwaleta pamoja waasi wa Afghanistan katika meza ya mazungumzo, amekumbusha mwandishi wetu katika katika mji wa Islamabad, Michel Picard.

Kisha Marekani. Nchi hii ina wanajeshi 9800 kwa jumla ya askari 13 000 wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO nchini Afghanistan, Marekani inabeba sauti na kuleta udhamini wa jumuiya ya kimataifa. China, nchi yenye nguvu katiika ukanda huo, kwa upande wake inahusika na kusimamia kile kinachoweza kutokea baadaye katika ukanda huo.

Kwa upande wa serikali dhaifu ya Afghanistan, ambayo haina uwezo bila msaada kutoka nje kudumisha umoja na utulivu nchini humo, itashirikiana na pande hizo tatu ili kuimarisha uaminifu wake katika uwanja wa mapambano. Uhalali ambao unadhoofishwa na mashambulizi makubwa katika miezi ya hivi karibuni. Kundi la Taliban linalodhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35% ya Afghanistan linanaonekana kuwa limepata nafasi ya kipekee tangu lilipoondolewa madarakani mwaka 2001.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.