Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Blinken akutana na Erdogan na kuomba msaada zaidi wa kibinadamu

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken amekutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumamosi Januari 6, wakati wa hatua ya kwanza ya ziara yake Mashariki ya Kati, na kusisitiza "haja ya kuongeza misaada ya kibinadamu".

Moshi ukipanda juu ya majengo katika mji wa mpakani wa kusini mwa Lebanon wa Blida kufuatia shambulio la bomu la Israel, Januari 6, 2024, huku kukiwa na mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Moshi ukipanda juu ya majengo katika mji wa mpakani wa kusini mwa Lebanon wa Blida kufuatia shambulio la bomu la Israel, Januari 6, 2024, huku kukiwa na mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na rais wa Uturuki siku ya Jumamosi mjini Istanbul, akianza ziara mpya ya kikanda ambayo itampeleka hasa Israel, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa pamoja na Qatar, ili kusihi kuunga mkono ongezeko la misaada kwa Gaza na kuzungumza kuhusu njia za kuepuka kuenea kwa uhasama katika kanda nzima, miezi mitatu baada ya kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas.

■ Katika siku ya 91 ya vita kati ya Israel na Hamas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anataka kupunguza shinikizo, huku Hesbollah ya Lebanon ikilenga kambi ya kijeshi nchini Israel,kwa kujibu mauaji ya naibu kiongozi wa Hamas, wakati wa shambulizi huko Beirut unaohusishwa na Israel.

■ Siku ya Jumamosi, Hezbollah ya Lebanon ilirusha makumi ya makombora kuelekea kambi ya kijeshi kaskazini mwa Israel, shambulio lililowasilishwa kama jibu lake la kwanza kwa mauaji ya kiongozi na mbili wa Hamassiku ya Jumanne karibu na Beirut.

■ Ukanda wa Gaza “umekuwa tu usioweza kukaliwa na watu”, na wakazi wake “wanakabiliana na vitisho vya kila siku mbele ya macho ya ulimwengu”, amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, siku ya Ijumaa.

■ Kulingana na ripoti mpya iliyotangazwa Jumamosi Januari 6 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 22,722 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Kuna karibu watu 60,000 waliojeruhiwa. Siku ya Alhamisi jeshi la Israel lilisema kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 8,000 wa Kipalestina tangu shambulio la Oktoba 7. Wanajeshi 175 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza Oktoba 27, kulingana na takwimu za hivi punde za jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.