Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI

Takwimu Mpya za Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa UN zaonesha zaidi ya watu 5,000 wamepoteza maisha nchini Syria

Zaidi ya watu elfu tano wamepoteza maisha nchini Syria tangu kuzuka kwa machafuko katika taifa hilo yaliyodumu kwa zaidi ya miezi tisa sasa Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia Haki za Binadamu ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN.

REUTERS/Omar Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

Navi Pillay amesema licha ya takwimu kuonesha kuwa watu zaidi ya elfu tano wameshapoteza maisha kuna kila dalili za kuongezeka kwa vifo hivyo katika siku za usoni iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa kukomesha ghasia hizo.

Mkuu wa Tume hiyo ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa UN ameongeza kuwa wamebaini serikali ya Rais Bashar Al Assad inawashikilia zaidi ya wapinzani elfu kumi na nne na hakuna taarifa za uhakika iwapo bado wapo hai au la.

Pillay amewaambioa wanachama kumi na tano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha wapo watoto wanaokadiriwa kufikia mia tatuhuku zaidi ya watu elfu kumi na nne wanatajwa kukimbia nchi hiyo.

Pillay amewaambia wanachama hao kuwa idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka kila mwezi huku akilinganisha takwimu ambazo alizotoa mwezi August zilikuwa zinaonesha watu elfu tatu wamepoteza maisha lakini sasa kunaongezeka la zaidi ya vifo vya watu elfu mbili.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa UN Bashar Jaafari amepinga takwimu hizo na kumtuhumu wazi wazi Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu Pillay kuwa amekuja na taarifa ya kupotosha.

Balozi Jaafari ameongeza kuwa taarifa hiyo inaonesha wazi kabisa haikuwa na mizani na badala yake imetolewa kwa ajili ya kuendelea kuaminisha dunia ubaya ambao unafanywa na serikali ya Rais Assad.

Naye Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa UN Vitaly Churkin aliwalaumu baadhi ya wanachama kutokana na kutumia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kwa faida yao badala ya kutenda haki.

Urusi na China ndiyo nchi ambazo zimeendelea kupingana na maamuzi mengi ambayo yanapendekezwa na nchi wanachama wengine wa Baraza la Usalama ambao wanashinikizwa kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali dhidi ya Syria.

Machafuko nchini Syria yalianza mwezi Machi ukiwa ni muendelezo wa mwamko katika mataifa ya kiarabu kutaka kuondoka tawala zilizokuwa madarakani huku kilio kikubwa katika nchi hiyo kikiwa ni kupatikana kwa demokrasia ya kweli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.