Pata taarifa kuu
SYRIA-UFARANSA

Maandamano yaitishwa Nchini Syria wakati huu hofu ya kusitishwa moja kwa moja kwa mashambulizi na serikali ya Damascus ikiongezeka

Mpatanishi wa Kimataifa ya Umoja wa Mataifa UN na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kofi Annan amekosoa namna ambavyo serikali ya Syria ilivyoshindwa kutekeleza mapendekezo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililomraka kuondoa silaha zake nzito ambazo zimeendelea kuwepo mitaani.

Vifaru vya serikali ya Syria bikiwa vimeendelea kusalia katika mitaa mbalimbali ya Miji ya nchi hiyo
Vifaru vya serikali ya Syria bikiwa vimeendelea kusalia katika mitaa mbalimbali ya Miji ya nchi hiyo AFP/YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Annan anasema kuwa ni kweli nchi ya Syria imeweza kusitisha mapambano lakini imeshindwa kutekeleza pendekezo la kuondao silaha zake zilizopo kwenye maeneo yenye watu wengi kitu ambacho kinakwenda kinyume na mapendekezo sita yaliyotolewa ili kumaliza umwagaji wa damu uliodumu kwa miezi kumi na mitanu.

Kauli ya Annan inakuja wakati huu ambapo Wanaharakati nchini Syria wakisema kuwa kumeshuhudiwa mapambano kwa mara ya kwanza baina ya vikosi vya serikali na wapinzani ikiwa ni saa kadhaa baada ya serikali ya Rais Bashar Al Assad kutekeleza pendekezo la kusitisha kusitisha mapigano.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa UN Bashar Jaafari kwa upande wake ameshutumu wale ambao wanaendelea kuikosoa nchi hiyo katika harakati zake za kutekeleza mapendekezo sita ya Mpatanishi Annan katika kumaliza umwagaji wa damu katika nchi hiyo.

Upinzani nchini Syria kwa mara nyingine umeitisha maandamano makubwa kuendelea kudhihirisha iwapo kweli serikali ya Damascus imesitisha mapigano kwa dhati au itarejea tena kwenye mapigano na wapinzani.

Maelfu ya wananchi wanaounga mkono upinzani wamehamasishwa kujitokeza baada ya sarat Ijumaa kuendelea kupaza sauti yao ya kutaka mabadiliko ya utawala nchini Syria kitu ambacho kitatoa nafasi ya demokrasia kuchukua mkondo wake.

Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameonesha wasiwasi wake kama kweli serikali ya Rais Assad ipo tayari kusitisha mashambulizi hayo kwa dhati akiwa na imani huenda wakashambuliwa wapinzani wake wowote.

Umoja wa Mataifa UN unajiandaa kupeleka waangalizi wake nchini Syria kuendelea kuangalia hali ilivyo wakati huu serikali ya Damascus ikisema imesitisha mashambulizi yake dhidi ya wapinzani.

Machafuko yaliyodumu kwa miezi kumi na mitatu nchini Syria yamesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tisa hii kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja huo iliyozuru huko mara kadhaa kujionea hali halisi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.