Pata taarifa kuu
SYRIA-DAMASCUS

Baraza la Usalama la UN la laaani mashambulizi ya mabomu mjini Damascus Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN limelaani vikali amshambulizi mawili ya mabomu yaliyotekelezwa mjini Damascus nchini Syria na kuua watu zaidi ya hamsini na kujeruhi watu zaidi ya 400.

Moshi mkubwa ukiwa umetanda mjini Damascus mara baada ya shambulio la bomu hapo jana
Moshi mkubwa ukiwa umetanda mjini Damascus mara baada ya shambulio la bomu hapo jana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lililotekelezwa mjini Damascus limeelezwa kuwa ni shambulio la kwanza na kubwa kuwahi kutekelezwa na makundi ambayo yanaushutumu utawala wa rais Asad.

Wengi wa waliopoteza maisha ni wanafunzi na wafanyakazi wengine ambao wakati shambulio hilo linatekelezwa walikuwa wakielekea kwenye shughuli zao na wanafunzi wakielekea shuleni.

Baraza la Usalama limeagiza pande zinakinzana nchini Syria kuacha mara moja mashambulizi yanayolenga wananchi na kuonya kuwa kuendelea kufanya hivyo kutaendelea kufanya hali ya usalama nchini humo kuzorota zaidi.

Serikali ya Syria imelaani shambulio hilo na kuvituhumu vikundi vya kigaidi toka nchi jirani za kiarabu ambazo awali ziliapa kutekeleza mashambulizi dhidi ya utawala wa rais Asad.

Bomu hilo limeelezwa kuwa lililenga kulipua ofisi za usalama wa taifa nchini humo pamoja na wafanyakazi ambao walikuwa wakiingia kwenye jengo hilo.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imesema kuwa watu waliotekeleza shambulio hilo walitumia milipuko miwili iliyokuwa na ujazo wa kilo 1000 na kutumia magari mawili kutekeleza mashambulizi hayo.

Kiongozi wa msafara wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa walioko nchini humo Robert Mood amevitaka vikundi vyote ambavyo vinaendesha mashambulizi kama haya kuacha mara moja kulenga makazi ya watu.

Tayari kundi la Al-Qaeda limetoa mkanda wa video kueleza kuhusika kwake na shambulio hilo pamoja na mashambulizi mengine yaliyotekelezwa nchini humo kwenye miji ya Allepo na Homs.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.