Pata taarifa kuu
ALGERIA-MALI

Hofu yazidi kutanda baada ya mateka mwingine raia wa Marekani kuuawa nchini Algeria

Hofu imezidi kutanda kwa raia wa kigeni wanaoshikiliwa kama mateka nchini Algeria baada ya mateka mwingine ambaye ni raia wa Marekani kuthibitika kuuawa jana ijumaa. Serikali ya Marekani imethibitisha kifo cha raia wake huyo aliyetambuliwa kwa jina la Frederick Buttaccio katika tukio ambalo raia wengine wawili walifanikiwa kutoroka wakiwa salama.

csmonitor.com
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa waasi hao wenye uhusiano wa karibu na kundi la Al Qaeda alikaririwa na Shirika la Habari la Mauritania ANI akisema wanaendelea kuwashikilia mateka wengine saba wa kigeni katika jangwa la Sahara karibu na mpaka wa Libya.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bi Hilary Clinton amesema mateka hao bado wapo katika hatari na ametoa wito kwa serikali ya Algeria kuhakikisha inawaokoa mateka wengine wanaoendelea kushikiliwa na waasi.

Wakati huo huo viongozi mbalimbali duniani wameendelea kuwaonya waasi hao ambao wanalenga kulipiza kisasi kutokana na vikosi vya Ufaransa kufanya uvamizi wa kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wanaopambana na serikali ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.