Pata taarifa kuu
Korea kaskazini

Mjomba wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Jang Song-Taek anyongwa

Serikali ya Korea Kaskazini imesema imemnyonga Jang Song-Thaek ambae ni mjomba wa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Kim Jong-Un. Thaek ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa nchini humo amekabiliwa na adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya usaliti.

REUTERS/China Daily
Matangazo ya kibiashara

Serikali za Marekani na Korea Kusini zimelaani adhabu iliyotolewa kwa kiongozi huyo.

Jang Song-Thaek, mwenye umri wa miaka 67 alikuwa na majukumu makubwa katika serikali, na alikuwa na nafasi ya pili nchini baada ya mpwa wake, ambae ni kiongozi wa nchi hio Kim Jong-Un aliyechukua nafasi ya kuingoza Korea Kaskazini baada ya kifo cha baba yake Kim Jong-Il miaka miwili iliyopita.

Jang Song-Thaek, alikamatwa juma liliopita, akiwa mkutanoni, na kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi jana alhamisi adhabu ya kifo.

Mtuhumiwa alichukuliwa na serikali ya Korea ya Kaskazini kama mhaini baada ya kutaka kuipindua uongozi wa chama na serikali, ili aiweke Korea Kaskazini katika mfumo mwengine, ambao ni tofauti na ule wa kisoshalisti.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Korea ya Kaskazini KCNA, Jang alikiri mahakamani yeye mwenyewe kuhusika na makosa ya kupanga njama za kuipindua serikali, akiwasihi wenzake ambao alikua akishirikana nao kulishawishi jeshi la taifa.

Jang Song-Taek, alikua naibu mwenyekiti wa halmashauri ya ulinzi wa kitaifa, ambayo ni taasisi inayochukua maamuzi mkubwa nchini humo.

Kunyongwa kwa Thaek kunatafsiriwa kama mkakati wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kutaka kuimarisha utawala wake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.