Pata taarifa kuu
MISRI - MAREKANI

Serikali ya Marekani yawataka viongozi wa Misri kuwaacha huru waandishi wa habari wa kituo cha Aljazeera

Serikali ya Marekani imeendelea imewataka viongozi wa serikali ya Misri kuwaachia huru waandishi wa habari wa kituo cha kimataifa cha nchini Qatar cha Aljazeera wanazuiliwa katika jela moja jijini Cairo. Ikulu ya Marekani imesema inaguswa kwa karibu zaidi na swala hilo.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Juma lililopita makahama moja jijini kairo ilifahamisha kwamba jumla ya waandishi wa habari 20, wakiwemo wanne wa kigeni watahukumiwa baada ya kutuhumiwa kutangaza habari zisizokuwa na ukweli wowote.

Watetezi wa haki za binadamu waendelea kutiwa wasiwasi kuhusu kushuka kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini humo, na ambapo wananchi nchini humo hawapewi nafasi ya kujitetea.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jya Carney amesema Vikwazo juu ya uhuru wa kujieleza nchini Misri ni ni hali inayoendelea kutia mashaka, na kwamba pamoja na ukweli kwamba waandishi wa habari na wasomi, nchini humo na na nje ya nchi, wanalengwa na utawala kwa kosa tu la kutoa maoni yao.

Msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani amesema Watu hao bila kujali vituo vyao lazima walindwe na kuwa kuruhusu kufanya kazi kwa uhuru nchini Misri, na kuitaka serikali kuwaacha huru waandishi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.