Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-Ubadhirifu

Rais Jacob Zuma na mawaziri wengine katika serikali yake wakabiliwa na kashfa ya urasibu mbaya wa mali ya uma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ametakiwa kurejesha sehemu ya pesa za walipakodi ziliyotumiwa kwa ujenzi wa makaazi yake binafsi kijijini Nkandla (mashariki), ambayo haihusiane kabisa na usalama wake, amesema leo msuluhishi anaehusika na kupambana dhidi ya rushwa.

Raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa majengo yaliyojenwa na Zuma kwa rands milioni 246 (sawa na yuro milioni 16.5), ni pamoja na kituo cha mapokezi kwa wageni, jengo la mikutano, banda la kuku, bwawa la kuogea na mabanda mengine ya mifugo, amebaini msuluhishi Thuli Madonsela, huku zikisalia wiki saba ya chaguzi zitakazofanyika mei 7.

Gharama ziliyotumiwa na serikali ni nyingi mno ikilinganishwa n zile zilitengwa kwa min ajili ya usalama wa rais. Ni wazi kwamba pesa hizo zilitumiwa kwa fujo, amebaini Madonsela katika ripoti yake.

Msuluhishi huyo amebaini kwamba rais Jacob Zuma na mawaziri wengine katika serikali yake wamewajibika katika urasibu mbaya wa mali ya uma, huku akisema kwamba rais Zuma atapaswa kurejesha pesa aliyotumia kinyume cha sheria.

Katika ripoti hiyo, iliyowekwa hadharani leo, Thuli Madonsela, amemuomba rais Zuma kuzitaka kila wizara kueleza jinsi zilivyotumia mradi wa ujenzi wa makkazi yake, akibaini kwamba kulikueko na “ubadhirifu wa mali ya uma”.

Pesa ziliyotumiwa katika mradi uliyobatizwa Nkandla zilikua zinahusu tu kukarabati sehemu za katikati ya mji wa Durban na mradi wa kukabiliana na mmomonyoko wa aridhi, ambao umekua ukisababisha madhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.