Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-Ubadhirifu

Zuma : asema hakuomba kukarabatiwa nyumba yake

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amethibitisha kwenye televisheni moja ya Afrika Kusini, kwamba hakuomba utumiaji wa mamilioni ya pesa za Uro ziliyolipwa na walipakodi katika ujenzi wa makaazi yake ya Nkandla (mashariki), na kubaini kwamba hatolipa pesa hio.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Kirsty Wigglesworth/PA
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyotolewa machi 19, msuluhishi anaehusika na kitengo cha kupambana na rushwa,Thuli Madonsela, aliamua kwamba kiwango cha randi milioni 246 (sawa na Uro milioni 16.5) kilitumiwa katika shughuli za ujenzi wa makaazi ya Jacob Zuma, na kuamuru Zuma arejeshe nusu ya kiwango hicho, akibaini kwamba kuna baadhi ya vitu viliyowekwa kwenye makaazi hayo, ambavyo havihusiane na usalama wake.

Akizungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusiana na ripoti hio, Zuma ametupilia mbali kuhusika kwa serikali na ujenzi huo.

“Waliyofanya hivo hawakunishirikisha, vipi nilipe kitu ambacho sijaomba wanifanyiye”, amesema Zuma kwenye televisheni moja ya kibinafsi ya ANN7.

Rais Zuma, ambaye anagombea muhula mwengine, ameyasema hayo, akishawishi raia wa mji wa Gugulethu wampigiye kura katika chaguzi za mei 7.

Chama madarakani cha ANC, kilimtetea hivi karibuni rais jacob Zuma na kuomba waliyohusika na ujenzi wa jengo la “Nkandla-gate”, wafuatiliwe, hata kama itakuwa ni wafanyakazi wa serikali, mawaziri, waliyokuwa mawaziri na mafundi.

Kwa upand wake, chama kikuu cha upinzani (DA), kimesema kitawafugulia mashtaka wafanyakazi wote waliyohusika katika ujenzi jengo hilo la Nkandla. “Tunapaswa kujitenga na watu wanaochafua taifa hili kwa rushwa.

Chama cha rais Zuma cha ANC kinajihusisha na rushwa, na ni lazima kirejeshe mali ziliyopotea, na kinapaswa pia kushindwa katika chaguzi za mei 7”, chama hicho kikuu cha upinzani kilifahamisha hivi karibuni katika taarifa kiliyotoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.