Pata taarifa kuu

DRC: Mawaziri watatu wanaoegemea upande wa mwanasiasa Moise Katumbi wajiuzulu

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mipango, Mwando Nsimba, Waziri wa Uchukuzi Chérubin Okendé na Naibu Waziri wa Afya Véronique Kilumba Nkulu.

Moïse Katumbi, kiongozi wa chama cha "Ensemble pour la République" nchini DRC.
Moïse Katumbi, kiongozi wa chama cha "Ensemble pour la République" nchini DRC. © RFI/France24
Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu huku kunafuatia hasa kuondoka kwa Moïse Katumbi na kundi lake la kisiasa la Umoja wa Kitakatifu, ambapo hivi karibuni aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba mwakani.

Mwaka 2015, wakati wa mtengano na rais Joseph Kabila, wanachama kadhaa wa serikali pia waliondoka serikalini na kuunda G7 mnamo 2015.

Wakati huo huo, mkuu wa serikali ameitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri. Vyanzo vya habari vilivyo karibu na ikulu ya rais vikieleza kuwa mabadiliko ya baraza la mawaziri ilikuwa ajenda ya mkutano huo.

Wakati huo huo Momat Kabulo Christian, Waziri wa Mipango na Bajeti wa jimbo la Haut-Katanga amewasilisha Jumatano hii, Desemba 28 barua yake ya kujiuzulu kwa gavana wa jimbo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.