Pata taarifa kuu

Guterres alaani vikali shambulio la wanajihadi katika shule ya upili nchini Uganda

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres 'analaani vikali' shambulio la wanajihadi kwenye shule ya upili magharibi mwa Uganda lililosababisha vifo vya takriban watu 41, amesema mmoja wa wasemaji wake siku ya Jumamosi Juni 17. 

Wanafunzi 25 wameripotiwa kuawaua katika shambulio la ADF nchini Uganda mpaka na DRC
Wanafunzi 25 wameripotiwa kuawaua katika shambulio la ADF nchini Uganda mpaka na DRC © FMM
Matangazo ya kibiashara

"Wale waliohusika na kitendo hiki cha kutisha lazima wafikishwe mahakamani," Farhan Haq amesema. Bw. Guterres pia anatoa wito wa "kuachiliwa mara moja" kwa wale waliotekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu, ameongeza.

Takriban watu 41 wameuawa, wengi wao wakiwa wanafunzi, katika uvamizi uliofanywa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi Juni 17 na wanajihadi dhidi ya shule, shambulio baya zaidi la aina hii kuwahi kutokea nchini Uganda kwa miaka mingi.

Maafisa wa jeshi na polisi wamewalaumu wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF), wanamgambo wa Kiislamu ambao walitangaza kuwa sehemu ya kundi la Islamic State, baada ya shambulio la umwagaji damu katika shule ya sekondari wilayani Kasese, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa upade wake Ufaransa imelaani kitendo hicho ilichokiita cha 'kikatili' dhidi ya shule ya upili magharibi mwa Uganda, ambalo limesababisha vifo na majeruhi kadhaa, kulingana na taarifa ya Jumamosi na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje.

"Ufaransa inatuma rambirambi zake kwa familia na ndugu, jamaa na marafiki wa wahanga, kwa mamlaka ya Uganda na kuelezea mshikamano wake na waliojeruhiwa," ameongeza msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.