Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Uganda: baadhi ya miili ya waliofariki katika shambulizi la Juni 17 bado haijatambuliwa

Familia za wahanga wa shambulizi dhidi ya shule ya sekondari, kitendo kilichotekelezwa na waasi wa ADF na kusababisha vifo vya watu 43 usiku wa Juni 16 kuamkia 17 katika mji wa Mpondwe wilayani Kasese, mpakani na DRC, wanaendelea kuomboleza. Lakini zaidi ya wiki moja baada ya shambulio hilo, wengine bado wana mashaka.

Ndugu na jamaa wanaomboleza vifo vya Florence Masika na mwanawe Zakayo Masereka, ambao wote waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF kwenye Shule ya Sekondari ya Lhubiriha, wakati wa mazishi yao huko Nyabugando, Uganda, Jumapili Juni 18, 2023.
Ndugu na jamaa wanaomboleza vifo vya Florence Masika na mwanawe Zakayo Masereka, ambao wote waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF kwenye Shule ya Sekondari ya Lhubiriha, wakati wa mazishi yao huko Nyabugando, Uganda, Jumapili Juni 18, 2023. AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Mpondwe, Lucie Mouillaud

Baada ya shambulio la mauaji katika shule alikokuwa akisomea mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 17, Kule Safati Mirundu alifanya anachoweza kujuwa wapi aliko mwanae.

“Mara moja nilienda hospitali, lakini mwanangu hakuwa miongoni mwa waliofariki. Baadaye, nilienda shule haraka, lakini miili ilichomwa hadi kiwango ambacho hatukuweza kutambua watoto zetu. »"

Jumla ya maiti 17 bado hazijatambuliwa, nyingi zikiwa zimepatikana katika bweni la wavulana wa shule hiyo. Kwa mujibu wa baba wa familia, jambo gumu zaidi ni kutojua ikiwa mtoto wangu alikufa wakati wa shambulio hilo, au ikiwa alitekwa nyara na washambuliaji akiwa na wanafunzi wengine. " Ninajisikia vibaya. Hata sasa sijisikii hasa kwa vile sielewi kilichompata mwanangu ikiwa ni miongoni mwa waliotekwa nyara au waliochomwa moto. Hata sasa, mama yake yuko kitandani, mgonjwa kwa huzuni, kwani hajui ikiwa mtoto wake atazikwa kwa heshima au la. "

Waziri wa Habari wa Nchi, Goddfrey Kabbyanga alisema kutoka Mpondwe Jumatatu kuwa wanafunzi watatu walitekwa nyara na ADF. Kuhusu maiti ambazo hazijatambuliwa, uchunguzi unaendelea vizuri, alisema Luteni Mate Magwara, mmoja wa maofisa usalama wa wilaya hiyo.

“Tulileta miili hiyo Fort Portal, ambako polisi wanafanya uchunguzi wa DNA ili kubaini ndugu wa kila marehemu, ili waweze kuzikwa ipasavyo. "

Matokeo ya kwanza ya vipimo vya DNA lazima yarejeshwe siku ya Jumanne, na sehemu ya miili, ikishatambuliwa, iikabidhiwe moja kwa moja kwa ndugu zao.

Katika eneo la shambulio hilo, magofu ya shule hiyo yanaonyesha shambulio la kundi la waasi, lenye asili ya Uganda lakini lililoko mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miaka ishirini.

Kwa jumla, majengo matatu ya shule yalichomwa na washukiwa wa ADF, mabweni mawili na chumba cha kuhifadhia vitu. 

Kulingana na mamlaka, shambulio la mwisho la ADF katika eneo hili lilifanyika mwezi Novemba 1996. Huku takriban watu hamsini wakiuawa, inachukuliwa kuwa ni shambulio la kwanza kabisa la kundi la waasi lililoundwa miaka michache mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.