Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Idadi ya waliouawa katika shule ya upili Uganda yongezeka, upinzani wakosoa mamlaka

Nchini Uganda, idadi ya waliouawa katika shambulizi la kigaidi katika shule ya upili magharibi mwa nchi hiyo imefikia 43. Wakati huo huo, upinzani unaendelea kuikosoa serikali, hasa juu ya uwezo wa usalama nchini Uganda.

Waombolezaji wakikusanyika kwa ajili ya mazishi ya Florence Masika na Zakayo Masereka wakati wa ibada ya mazishi yao huko Mpondwe Juni 18, 2023.
Waombolezaji wakikusanyika kwa ajili ya mazishi ya Florence Masika na Zakayo Masereka wakati wa ibada ya mazishi yao huko Mpondwe Juni 18, 2023. AFP - STUART TIBAWESWA
Matangazo ya kibiashara

Nchini Uganda, idadi ya watu waliouawa inaongezeka baada ya shambulio la kigaidi lililotekelezwa usiku wa Juni 16 kuamkia Juni 17, 2023 karibu na mpaka wa DRC, katika shule ya upili ya Mpondwe. Mamlaka inashutumu kundi la Kiislamu la ADF kwa kuhusika na shambulio hilo ambalo, kulingana na vyombo vya habari vya Uganda, sasa limegharimu maisha ya watu 43 kufuatia kifo cha mmoja wa waliojeruhiwa.

Wakati huo huo, usalama umeimarishwa magharibi mwa nchi. Kwa ombi la Rais Yoweri Museveni, wanajeshi zaidi wametumwa atika eneo hilo, hasa karibu na Milima ya Rwenzori, ambapo Allied Democratic Forces (ADF) walikuwa wameanzisha uasi wao katika miaka ya 1990, na ambapo kundi hilo linaendesha kilimo cha kakao na uchimbaji madini.

Operesheni ya kuwasaka washambuliaji hao pia inaendelea katika nchi jirani ya Congo ambako magaidi hao wanasemekana kutorokea. Wanafunzi watatu wa shule ya upili waliokuwa wanashikiliwa na kundi hilo kwa kubeba vyakula vilivyoibiwa, pia wamefanikiwa kutoroka. Wamerudishwa kwa familia zao, jeshi limesema.

"Walikuwa kati ya 5 na 10. Sasa wako katika Hifadhi ya Virunga na tunajaribu kuwaondoa katika Hifadhi hiyo, kulingana na Felix Kulayigye, msemaji wa jeshi la Uganda. Mapigano yamezuka kati ya wanajeshi wetu na magaidi hao. Tuliwaokoa wanafunzi watatu na mwanamke mmoja na watoto wawili waliokuwa wametekwa nyara na kundi hilo, lakini hatujui ni wapi. ADF bado inawashikilia vijana wetu watatu. Kwa hivyo misheni yetu inaendelea hadi tuwakomboe. "

Mshukiwa mmoja pia amekamatwa. Kijana ambaye alikuwa amechapisha video kwenye TikTok akisema kwamba ni mpiganaji wa ADF na kwamba alishiriki katika shambulio dhidi ya shule hilo la upili.

Upinzani unaendelea kuikosoa serikali. Kulingana na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani, shambulio hilo linaweza kuwa kulipiza kisasi kwa kundi hilo baada ya wanajeshi wa Uganda kushiriki katika operesheni dhidi yake nchini DRC. Madai ambayo Brigedia Jenerali Kulayigye anakanusha: “Shambulio la Pondwe lilikuwa la fursa. Lengo ni kuwarejesha wanajeshi wetu nchini Uganda, kwa sababu ya shinikizo wanalopata DRC. Sio kulipiza kisasi. DRC si nchi yao, hivyo hawawezi kulipiza kisasi kwa nchi ambayo wao wenyewe ni wageni. »

Mnamo Juni 21, mpinzani Abdallah Kiwanuka alibaini kwamba kutumwa kwa jeshi nje ya nchi kumepunguza uwezo wa usalama nchini Uganda. Ametoa wito kwa mamlaka kuamuru kurejea nchini kwa wanajeshi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.