Pata taarifa kuu

Uganda: Mwanamke ajifungua mapacha akiwa na umri wa miaka 70

Mwanamke wa Uganda mwenye umri wa miaka 70 amejifungua mapacha, "jambo lisilo la kawaida", kulingana na Edward Tamale Sali, daktari, ambaye alifuatilia ujauzito wake hadi kujifungua.

(picha ya kielelezo)
(picha ya kielelezo) © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mama huyo, Safina Namukwaya amepata mapacha baada ya kupata ujauzito kupitia matibabu ya kupandikiza (IVF), na kuwa mwanamke mzee zaidi barani Afrika kujifungua, kwa mujibu wa hospitali alikopata watoto.

Mama huyo, Safina Namukwaya, ameeleza kuzaliwa kwa mapacha hao mvulana na msichana kuwa ni “muujiza” siku ya Jumatano.

Mama na watoto wako katika afya njema na bado wako chini ya uangalizi katika kituo kimoja cha afya katika mji mkuu Kampala, ameongeza Edward Tamale Sali. Safina Namukwaya kwa kawaida anaishi kijijini Masaka, takriban kilomita 120 magharibi mwa mji mkuu.

Mwanamke huyo wa umri wa miaka 70 alijifungua mtoto wa kike miaka mitatu iliyopita, baada ya kutajwa kuwa "mwanamke aliyelaaniwa" kwa kushindwa kupata watoto hapo awali.

Akiwa na mume wake wa kwanza, ambaye alikufa mwaka wa 1992, hakuwa na mtoto. Mpenzi wa sasa wa Bi Namukwaya, ambaye alikutana naye mwaka wa 1996, hata hivyo, hakwenda kumuona mkewe alipojifungua, jambo ambalo halikumshangaza mama huyo. "Labda hajafurahi kwa kuwa nilijifungua mapacha ... kwa kuogopa majukumu yatakayomkabili," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.