Pata taarifa kuu

DRC : MONUSCO imewaondoa wanajeshi wake katika kambi ya Kamanyola

Nairobi – Umoja wa Mataifa, hapo jana Jumatano umeanza kuwaondoa wanajeshi wa tume yake ya kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, ambapo wamekabidhi rasmi kambi ya kwanza iliyokuwa chini ya vikosi hivyo kwa jeshi la polisi.

Hivi karibuni Monusco itajiondoa pia kwenye maeneo ya Uvira, Mikenge, Bunyakiri, Bukavu na kwengineko
Hivi karibuni Monusco itajiondoa pia kwenye maeneo ya Uvira, Mikenge, Bunyakiri, Bukavu na kwengineko © Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Hafla hiyo ilifanyika kwenye kambi ya Monusco huko Kamanyola eneo la Rubumba.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo Bintou Keita amesema makabidhiano ya kambi hiyo kwa mamlaka ya Congo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kujiondoa kwa Monusco nchini humo kulingana na barua ya pamoja iliyotiwa saini mnamo Novemba 21 mwaka jana kati ya serikali ya Congo na MONUSCO.

Kamanyola ni kituo cha kwanza cha Monusco Kivu kuzini kinachofunga baada ya barua ya pamoja iliyotiwa saini mnamo Novemba 21 mwaka jana kati ya serikali ya Congo na MONUSCO iliyohusiana na kujiondoa kwa Monusco kwa utaratibu, kuwajibika na kwa hatua kwa hatua kutoka DRC”. alisema Bintou  Keita .

00:22

Bintou Keita- Mkuu wa Monusco nchini DRC

Kambi hii ya Monusco imekuwa ikitumika huko Kamanyola tangu mwaka 2005, askari 112 wakiwa tayari wameondoka wengine 2000 wakitarajiwa kuondoka kivu kusini ifikapo mwishoni mwa mweDRzi Aprili. 

Alipokabidhiwa funguo za kambi hiyo, gavana wa muda katika jimbo la Kivu kusini Marc Malago alizikabidhi baadae kwa polisi akiwataka kuwa na nidhamu nakuishi kwa uhusiano bora na wakazi.

Walinda amani wa UN wamekuwa wakituhumiwa kwa kushindwa kuwajibikia wajibu wao.
Walinda amani wa UN wamekuwa wakituhumiwa kwa kushindwa kuwajibikia wajibu wao. © Glody Murhabazi / AFP

Marc Malago ameahidi kwamba juhudi zitazidishwa kuboresha ulinzi wa raia na mali zao.Baadhi ya raia Kamanyola wamekuwa na mtazamo huu kuhusu hatua hii.

Aidha mkuu wa MONUSCO Bintou Keita ameeleza kwamba baada ya kuondoka kwa MONUSCO, Umoja wa Mataifa utasalia nchini Congo kupitia mashirika yake ili kuendeleza msaada wa Umoja wa Mataifa Congo, kulingana na mamlaka yake.

Hivi karibuni Monusco itajiondoa pia kwenye maeneo ya Uvira, Mikenge, Bunyakiri, Bukavu na kwengineko.

William Basimike, Bukavu, RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.