Pata taarifa kuu

RDC: Mukwege ameitaka UN kutowaondoa wanajeshi wa MONUSCO

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2018 Daktari Denis Mukwege, ameliandikia barua, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kulitaka kufuta mpango wake wa kuondoa jeshi la kulinda amani MONUSCO nchini humo kufikia mwisho wa mwaka huu.

Badala ya kuondoka, Mukwege amelipendekezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kubadilisha utaratibu wake wa operesheni nchini DRC
Badala ya kuondoka, Mukwege amelipendekezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kubadilisha utaratibu wake wa operesheni nchini DRC Getty Images via AFP - RICCARDO SAVI
Matangazo ya kibiashara

Mukwege, ambaye pia ni mwanasiasa aliyewania urais mwaka ulioipita na kushindwa na rais Felix Thisekedi, amesema kwenye barua yake kuwa, ombi lake linatokana na kuendelea kwa utovu wa usalama na hali mbaya ya kibinadamu,jimboni Kivu Kasakazini.

Aidha, amesema kwa sasa sio muda mwafaka wa kukiondoa kikosi cha MONUSCO kwa sababu maisha ya raia hasa wa Mashariki yatakuwa kwenye hatari na kuondoka kwa kikosi hicho kitasababisha hali ya usalama kuwa mbaya zaidi.

MONUSCO imeanza kuondoka nchini DRC baada ya utawala wa Kinshasa kuwataka kuondoka.
MONUSCO imeanza kuondoka nchini DRC baada ya utawala wa Kinshasa kuwataka kuondoka. © Photo MONUSCO/Force

Badala ya kuondoka, Mukwege amelipendekezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kubadilisha utaratibu wake wa operesheni nchini DRC ili kuweka mazingira yatakayowezesha jeshi la DRC kuwa imara na kujihami vilivyo, kabla ya kukosi cha UN kuondoka.

Barua hii ya Mukwege imekuja baada ya wiki iliyopita, MONUSCO kufunga kambi yake ya Kamanyola, jimboni Kivu Kusini, ili kuanza safari ya kuondoka nchini humo baada ya kuwepo kwa miaka 25.

Mwaka uliopita, rais Felix Tshisekedi aliliambia Umoja wa Mataifa, kuanza kuondoka vikosi vyake nchini mwake, baada ya kushindwa kuwatokomeza makundi ya waasi, Mashariki mwa nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.