Pata taarifa kuu

Kenya yasitisha mpango wake wa kutuma polisi nchini Haiti

Kenya imeamua kusitisha mpango wa kutuma maafisa wa polisi nchini Haiti, kama sehemu ya ujumbe wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, amesema afisa mkuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

Watu hukimbia gesi ya kutoa machozi wanapoandamana kupinga kupanda kwa gharama ya maisha huko Petit-Goâve, Haiti, Septemba 14, 2023.
Watu hukimbia gesi ya kutoa machozi wanapoandamana kupinga kupanda kwa gharama ya maisha huko Petit-Goâve, Haiti, Septemba 14, 2023. © Richard PIERRIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani imejibu mara moja: Wizara ya Mambo ya Nje imesema haikuona sababu ya kuchelewesha mpango huu wa kutuma maafisa wa polisi nchini Haiti.

"Kumekuwa na mabadiliko makubwa kufuatia kuzorota kabisa kwa utulivu wa umma na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti" Ariel Henry, Korir Sing'oei, katibu kiongozi katika Wizara ya Mambo ya  Nje ya Kenya, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Bila ya utawala wa kisiasa nchini Haiti, hakuna mahali pa msingi ambapo kikosi cha polisi kinaweza kupumzika, kwa hivyo serikali (ya Kenya) itasubiri kutangazwa kwa mamlaka mpya ya kikatiba nchini Haiti kabla ya kuchukua "maamuzi zaidi kuhusu suala hilo," ameongeza.

Ameongeza kuwa Nairobi, hata hivyo, iko tayari "kutoa uongozi" kwa ujumbe wa kimataifa, ambao uliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba.

Kenya ilikuwa imesema iko tayari kutuma maafisa wa polisi elfu moja nchini Haiti, inayokumbwa na machafuko kutokana na mapigano kati ya polisi na magenge yenye silaha, lakini mradi huu ulikumbana na vikwazo vingi vya kisheria nchini Kenya.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry, ambaye magenge yenye silaha na baadhi ya raia wamekuwa wakidai ajiuzulu, ametangaza siku ya Jumatatu jioni kwamba anaachia ngazi, wakati nchi hii maskini ya Caribbean iko katika mzozo mkubwa wa usalama na kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.