Pata taarifa kuu
Burundi-Maadhimisho

Wananchi wa Burundi waadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha rais Cyprien Ntaryamira

Wananchi wa Burundi wameadhimisha hii leo kumbukumbu ya miaka 20 tangu kuawa kwa rais Cyprien Ntaryamira katika udunguaji wa ndege ilokuwa ikiwasafirisha na rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana jijini Kanombe huko Kigali.

Rais wa zamani wa Burundiu Cyprien Ntaryamira
Rais wa zamani wa Burundiu Cyprien Ntaryamira Frodebu.be
Matangazo ya kibiashara

Rais Cyprien Ntaryamira ambaye aliongoza Burundi katika kipindi kigumu cha machafuko ya wenyewe kwa wenyewe, aliuawa April 6 mwaka 1994 jijini Kigali akiwa katika ndege iliokuwa ikiwasafirisha yeye na mwenziwe wa Rwanda Juvenal Habyarimana wakati wakituwa kwenye uwanja wa ndege wa Kanombe wakitokea jijini Arusha nchini Tanzania.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika tarafa mbalimbali za mikoa ya Burundi ambako misaa ya maombolezo imeshuhudiwa katika kanisa mbalimbali.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki katika mkoa wa Bujumbura Monsignori Evariste Ngoyagoye amewataka waumini kupiga vita hali yoyote inayoweza kusabibisha kifo, huku akibaini kuwa Cyprien Ntaryamira akikufa kutokana na sababu za kisiasa. Kiongozi huyo amewataka waumini hao kumuomba Mungu sio tu kwa taifa la burundi lakini pia kuwaombea raia wa Rwanda juu ya harakati zao za kupiga vita hisia zinazo weza kusababisha kifo.

Miaka 20 tangu kutokea kwa mauji hayo ya rais wa Burundi pamoja na mawaziri wake wawili Cyriaque Simbizi na Bernard Ciza hakuna ukweli wowote uliowekwa bayana na serikali kuhusu mauaji hayo. Kiongozi wa chama cha hayati huyo cha Frodebu Leonce Ngendakumana amesema serikali ya Burundi inalojukumu la kufuatilia kesi hii ukizingatia kuwa Cyprien Ntaryamira alifariki akiwa rais wakati akitokea katika ziara ya kikazi kuhusu amani ya Burundi.

Leonce Ngendakumana amesema serikali ya Burundi inataka swala hilo liwasilishwe kwenye tume ya ukweli na maridhiano, jambo ambalo amesema chama cha Frodebu kinapinga hatuwa hiyo kwakuwa rais Ntaryamira amefia ugenini na hili ni swala la kidiplomasia, linaweza kutatuliwa na mahakama za Rwanda au mahakam za kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.