Pata taarifa kuu
Burundi-Diplomasia

Serikali ya Burundi yamfurusha mwanadiplomasia mwingine wa UN

Serikali ya burundi imemfukuza nchini humo mwanadiplomasia mwingine wa Umoja wa Mataifa Bnub ambaye imesema alikamatwa na silaha katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini Bujumbura, ikiwa ni mwanadimplomasia wa pili wa kitengo wa UN kufurushwa nchini Burundi kwa kipindi cha miezi miwili.

Rais Nkurunziza akimpokea mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu
Rais Nkurunziza akimpokea mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure amesema uongozi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini Bujumbura ulimkuta mwanadiplomasia Abednego Mutua raia wa Kenya na Magazine 2 zikiwa na risase 15 wakati akijiandaa na safari, taarifa iliotolewa kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa kabla ya kuchukuliwa hatuwa ya kupewa muda wa saa 48 kuondoka nchini Burundi, na hili haligusi hata kidogo uhusiano bora uliopo kati ya serikali na Umoja wa Mataifa.

Mshauri wa rais anaye husika na mawasiliano Willy Nyamitwe amefahamisha kuwa mwanadiplomasia huyo alikmamatwa na silaha Mei 25 wakati akijiandaa kwa safari kuelekea nchini Kenya.

April 17 serikali ya Burundi ilichukuwa hatuwa kama hiyo ya kumfurusha mwanadiplomasia wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa anaye husika na maswala ya Usalama Paul Debbie, baada ya kuvuja kwa taarifa kutoka Umoja huo kuhusu serikali ya burundi kuwapa silaha vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD wa Imbonerakure.

Serikali ya Burundi ililaani vikali taarifa hiyo iliozagaa kwenye vyombo vya habari na kuiita kuwa ni uvumi usiokuwa na msingi na ambao unania pekee ya kuipaka tope serikali.

Hata hivyo kiongozi mmoja wa Bnub ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema serikali ya Burundi inataka tu kulipiza kisase baada ya kuvuja kwa taarifa hizo, kwa sababu Mutua ni kiongozi wa Usalama ambaye anaruhusiwa kumiliki silaha, na hakuwa tu muangalifu kwa kusafiri na silaha,

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.