Pata taarifa kuu
ALGERIA

Idadi ya watu waliokufa katika operesheni ya kuwaokoa mateka kwenye kituo cha Gesi nchini Algeria yafikia 80

Idadi ya watu waliokufa kutokana operesheni iliyokuwa inafanywa na kikosi maalumu cha askari wa Algeria kwenye kituo kimoja cha Gesi kusini mwa nchi hiyo imeongezeka na kufikia zaidi ya 80, maofisa usalama nchini humo wamethibitisha. 

Eneo la kiwanda cha Gesi ambacho kilitekwa na waasi wa Kiislamu mwishoni mwa juma nchini Algeria
Eneo la kiwanda cha Gesi ambacho kilitekwa na waasi wa Kiislamu mwishoni mwa juma nchini Algeria REUTERS/Kjetil Alsvik
Matangazo ya kibiashara

Kikosi maalumu cha uteguaji mabomu kimekuwa kkifanya uchunguzi wa iina kwenye kituo hicho kutafuta vifaa vya mlipuko ambapo wamekuta miili mingi ya watu ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kukaa muda mrefu.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi nchini humo amesema kuwa mara baada ya kuwasili kwa kikosi hicho ya kutegua mabomu wamekuta miili zaidi ya mateka ambao wanadaiwa kuuawa wakati watekaji hao wakiislamu walipokuwa wanawashikilia kama mateka.

Siku ya Jumamosi kikosi cha makomandoo wa Algeria kililazimika kutumia nguvu zaidi kuingia kwenye majengo ya kiwanda hicho kwa lengo la kumaliza siku nne za watu kushikiliwa mateka na makundi ya waislamu waliokuwa wanalaumu nchi ya Ufaransa kuingilia kijeshi taifa la Mali.

Wakati wa operesheni hiyo juma ya raia wa kigeni 31 wameripotiwa kuuawa sita wakitajawa kuwa ni raia wa Uingereza jambo ambalo mataifa ya magahribi yaliyokuwa na raia wake kwenye kiwanda hicho wakitaka maelezo ya kutosha kutoka kwa serikali ya Algeria.

Licha ya kufanikiwa kuwaokoa baadhi ya mateka wengi wamejeruhiwa huku waliouawa miili yao ikishindwa kutambulika kutokana na kuharibika vibaya baada ya kuuawa na watekaji nyara.

Nchi za Uingereza, Ujerumani na Marekani zimelaani shambulio hilo huku wakitaka Serikali ya Algeria kuongeza usalama kwa raia wake wanaofanya kazi nchini humo na kuahidi kushirikiana nayo katika kuhakikisha wanatokomeza ugaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.